Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Anang’ang’ania eti tuishi pamoja na mama mkwe!
SWALI: Za kwako shangazi. Mpenzi wangu anataka tukae na mama yake baada ya harusi. Mimi sitaki sababu najua tabu za mama mkwe. Nifanyeje?
Jibu: Hili ni jambo kubwa linalohitaji mazungumzo ya wazi kabla ya ndoa. Elezea kwa heshima lakini kwa uthabiti kwamba unahitaji nafasi yenu binafsi baada ya harusi.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO