Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Fikra za ‘ex’ zanitatiza nikiwa na mpenzi wangu
Mwanaume akiwa na msongo wa mawazo. Picha|Maktaba
SWALI: Kwako shangazi. Nilipata mpenzi mwingine mwezi uliopita baada ya wangu wa kwanza kuniacha. Juzi alitaka huduma za chumbani lakini nikashindwa kwa sababu bado namfikiria aliyeniacha. Nahofia yeye pia ataniacha. Nifanye nini?
Jibu: Huwezi kumsahau ghafla mtu uliyempenda kwa dhati. Vunja uhusiano huo kisha ungoje hadi umtoe moyoni mpenzi wako wa awali ndipo utafute mwingine.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO