Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Hataki kutumia kinga tukishiriki mapenzi
SWALI: Vipi shangazi? Mpenzi wangu hataki kutumia kinga. Anadai tukipendana kwa dhati hatupaswi kutumia kinga. Mimi nahofia afya yangu na kupata mimba kwani hatujaoana rasmi. Je, ni kosa kutilia shaka mapenzi yake?
Jibu: Hiyo si dalili ya upendo, ni kutojali. Afya yako ni muhimu kuliko maneno matamu. Mapenzi ya kweli hulinda, hayalazimishi. Ukiona hataki kinga, linda nafsi yako.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO