Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mke hajui kupika
Picha ya mtu akipika. Picha|Hisani
SWALI: Kwako shangazi. Nimekuwa na mke kwa mwaka mmoja sasa. Mke wangu ananiridhisha kwa mambo yote isipokuwa moja tu! Hajui kupika na nimemshindwa kumwambia. Naomba ushauri wako.
Jibu: Usithubutu kumwambia kwa sababu utaumiza nafsi yake. Lakini pia usiendelee kuumia. Tafuta namna umpeleke kwa masomo ya upishi. Mwambie ujuzi zaidi wa kupika utaleta furaha na mapenzi zaidi nyumbani.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO