Shangazi Akujibu                                                
                                            
                                        SHANGAZI AKUJIBU: Mke wangu anapuuza majukumu ya nyumbani sababu ya biashara
 
                                                    
                                                        Mwanamke akifanya kazi za nyumbani. Picha| Maktaba.                                                    
                                                SWALI: Tangu mke wangu aanze biashara, hanipi tena muda. Ameniachia majukumu yote ya nyumbani. Nikizungumza naye anasema simwelewi. Nifanye nini?
JIBU: Ndugu, dunia imebadilika—wanawake nao wanakimbizana na kazi na biashara kama wanaume. Usimlaumu moja kwa moja, bali tafuteni njia ya kuhakikisha kuwa hakuna anayevunjwa na majukumu ya nyumbani. Msaidiye pale inapoweza, kisha muweke ratiba. Ndoa si mashindano ya nani anafanya zaidi, bali ushirikiano.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO