Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi anataka tuishi pamoja kabla ya ndoa

Na SHANGAZI October 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Hujambo shangazi. Mpenzi wangu anataka tuishi pamoja kabla tuoane rasmi akisema ni njia ya kujuana vizuri kabla ya kuoana, lakini wazazi wangu hawajakubali. Niko njia panda. Naomba ushauri.

Jibu: Dada ushawishi huo ni wa kawaida siku hizi, lakini kumbuka: kuishi pamoja si ndoa. Kama anataka mjuane zaidi, basi mwambie aje na wazee kwenu. Mwanaume anayehofia ndoa ila ana haraka ya kuishi nawe, ana mpango wake binafsi.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO