Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi hutaka tushiriki hata nikiwa nimechoka
Wanandoa ambao wamekosa kuelewana kuhusu kushiriki tendo la huba. Picha|Maktaba
SWALI: Shikamoo shangazi. Kila tukipatana, ampenzi wangu nataka tushiriki mapenzi hata kama sina hamu. Nikikataa anasema simjali. Nifanyeje?
Jibu: Hilo si mapenzi, ni ukatili. Tendo la ndoa ni makubaliano, si amri. Mweleze wazi kuwa mwili wako ni wako, na hakuna anayepaswa kukulazimisha. Kama hataki kuelewa, huyo si mpenzi, ni mnyanyasaji.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO