Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mume amezoeana na mjakazi, ninawashuku!

Na SHANGAZI November 1st, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kila mara mume wangu anacheka na mjakazi wetu na hata kutaniana kana kwamba mimi sipo. Nimeanza kuhisi kuna jambo kati yao. Nianzeje kuchukua hatua bila kuonekana mwenye wivu?

Jibu: Usifanye fujo, lakini usikae kimya. Onyesha mipaka kwa hekima. Mwanaume mwenye nidhamu anajua mipaka.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO