Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Nashindwa kabisa kumsamehe

Na SHANGAZI December 25th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Shangazi, kila nikimuona mume wangu nakumbuka mabaya aliyonitendea hapo nyuma. Japo ameomba msamaha mara kadhaa, bado nimeshindwa kabisa kumsamehe.

Jibu: Msamaha ni safari, haiji mara moja. Kama maumivu bado yapo, tafuta ushauri. Kuishi na chuki ni kama kubeba mzigo mgongoni.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO