Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Ni kweli ananicheza?

Na SHANGAZI November 20th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kwako shangazi. Nimegundua mpenzi wangu ananicheza. Juzi rafiki yangu alinitumia picha wakiwa pamoja. Nilimpigia simu mpenzi wangu akadai hiyo ni njama ya kututenganisha. Naomba ushauri wako.

Jibu: Picha uliyotumiwa si ushahidi wa kutosha kwamba mpenzi wako ana uhusiano wa kimapenzi na rafiki yako. Inawezeka kuwa rafiki yako anamtaka na anatafuta jinsi ya kuwatenganisha. Mtafute mpenzi wako akuelezee zaidi.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO