Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Nina mke kisirani balaa!
Picha ya wapenzi wawili baada ya ugomvi. Picha| Maktaba
SWALI: Vipi shangazi. Nimeolewa kwa miaka mitatu sasa ila sijaona maana ya ndoa. Nilidhani mke wangu angenipa furaha maishani ila najuta kumuoa kwani tunagombana karibu kila siku. Naomba ushauri wako.
Jibu: Wakati mwingine ni vyema wapenzi au wanandoa kukubali ukweli kuwa hawawezi kuwa pamoja kisha kuachana kwa amani. Mweleze mke wako unavyohisi na pia umshauri kuhusu talaka ikiwa unahisi huwezi kumvumilia zaidi.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO