Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Nina ujauzito ila mpenzi wangu hataki mtoto
Mwanamke mjamzito akilia. Picha|Maktaba
SWALI: Kwako shangazi. Nina ujauzito ila mpenzi wanu amesema hayuko tayari kuwa baba. Ananisisitiza niavye mimba, lakini mimi sitaki. Nifanyeje?
Jibu: Mwanaume anayekupenda ataheshimu uamuzi wako, si kukushinikiza uavye mtoto. Usikubali hofu ichukue nafasi ya utu. Mtoto hana kosa—kama hataki kuwa baba, wewe bado unaweza kuwa mama jasiri.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO