Shangazi Akujibu                                                
                                            
                                        SHANGAZI AKUJIBU: Ninayemmezea mate anampenda rafiki yangu
                                                    
                                                        Mfanyakazi wa kiume na kike ofisini. PICHA|HISANI                                                    
                                                SWALI: Hujambo shangazi. Nimegundua kuwa mwanaume ninayemmezea mate anampenda rafiki yangu. Hii imenifanya nipoteze matumaini na masuala ya mapenzi. Naomba unipe ushauri wako ushauri.
Jibu: Usihuzunike. Wakati mwingine maisha hutukumbusha kuwa si kila tunayetaka atatutaka. Huyo mwanaume si wa mwisho duniani. Jipende, na ufahamu kuwa anayekufaa yupo njiani.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO