Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Walikuja, wakaonja, wakahepa, sijaolewa
Wanandoa wanaofarakana kwa sababu ya mchezo wa huba. Picha|Maktaba
SWALI: Shikamoo shangazi. Nina miaka 38 na sijaolewa wala sina mpenzi. Wanaume waliodai kunipenda walionja asali kisha wakahepa. Jambo hilo linanisumbua sana moyoni na naelekea kukata takaa ya kupata mume. Nishauri.
Jibu: Si jambo rahisi kupata mpenzi wa dhati. Ni kawaida kupata na kupoteza wapenzi kabla ya kupatana na yule anayekufaa. Usiwe mwepesi wa kufungua mzinga wako kwani hiyo ndio shabaha ya wanaume wengi. Kuwa na subira.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO