Transfoma ya mume wangu inazimazima
Shangazi;
Mimi ni mwanamke wa miaka 50 na mume wangu ana miaka 60. Mzee ameishiwa na nguvu za kiume. Nataka kaka anayejua kunengua mauno kwani naskia ni shupavu chumbani. Lakini sitamuacha mume wangu.
Sijawahi sikia unenguaji mauno unahusishwa na ustadi kitandani. Kwa upande wa kupata huduma, unahatarisha ndoa na afya yako na mumeo. Jihadhari!
Tangu apate kazi ya hela anarudi usiku amelewa
Tangu nioe mke wangu miaka sita iliyopita amekuwa mtulivu na mwema. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni amekuwa mkorofi. Anaingia nyumbani usiku wa manane akiwa mlevi. Hii ilianza baada ya kupata kazi yenye donge nono kuniliko. Nataka talaka!
Sidhani anachofanya mkeo kimefikia kiwango cha kumpa talaka. Pengine ni mawasiliano tu mnayohitaji ili kurekebisha mambo.
Mume anajua kunipa mahaba ila mvivu ajabu
Shangazi, mimi ni mwanamke wa miaka 50. Nimeolewa lakini mimi ndiye nimekuwa nikikithi mahitaji ya familia yetu. Mume anajua mapenzi lakini mvivu kweli kweli. Nahitaji mume wa pili anisaidie kujiendeleze kimaisha.
Sheria ya Kenya inamruhusu mwanamke kuwa na waume wawili? Pili, umezungumza na mumeo kuhusu udhia wako?
Mke wangu ametekwa na filamu za ngono
Miaka kadhaa mimi na mke wangu tulikuwa tunatazama filamu za ngono ili kuimarisha mahaba. Hata hivyo, baada ya muda nilihisi zinatuathiri na tukaafikiana tuache kuzitazama. Hata hivyo, mke wangu ameshindwa kabisa kuziacha. Ninahofia kwamba nampoteza mke wangu. Nifanyeje?
Imethibitishwa na wataalam kwamba filamu hizi zina athari. Mkeo Atahitaji ushauri nasaha ili kukabiliana na shida hii.