Makala

SIHA NA LISHE: Manufaa ya kula nyama nyeupe

July 12th, 2019 2 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

NYAMA nyeupe ni nyama ambayo inakuwa na rangi nyeupe kabla ya kupikwa mara tu baada ya mnyama au ndege kuchinjwa. Kwa mfano, nyama ya kuku, bata, mbuni, ndege wote na samaki aina zote huwa nyeupe.

Nyama nyekundu ni ipi?

hii ni nyama ambayo ikichinjwa inakuwa na rangi nyekundu kabla ya kupikwa; kwa mfano ni nyama za wanyama kama kondoo, mbuzi, ng’ombe, na kadhalika huwa ni nyekundu.

Hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Nyama nyekundu ina lehemu ambayo hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri.

Hii husababisha viungo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua lehemu ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha.

Ugonjwa wa kisukari

Watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula.

Hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs

Huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa.

Wanasayansi wanaamini protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia kwa ugonjwa huu.

Kifafa

Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo; hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa.

Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.

Unene kupindukia

Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe. Unene na kitambi ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.

Jua faida hasa za nyama hii nyeupe ukilinganisha na ile nyekundu:

Upatikanaji wa virutubisho muhimu vya siku kwani nyama nyeupe ina mafuta kidogo, vitamini, protini na nguvu kwa ajili ya shughuli za kila siku.

Nyama hizi zina amino acid nyingi ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa seli za binadamu na ukuaji wa nywele kwa ujumla.

Nyama hizi zina mafuta kidogo sana ambayo sio hatari kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa mwili wa binadamu.

Nyama ya samaki ina kemikali inayoitwa omega 3 ambayo haitengenezwi na miili yetu lakini ni muhimu sana kwa kupunguza kiasi cha lehemu au cholestrol mwilini.

Nyama ya kuku ina kiasi kikubwa cha selemium ambayo ina kazi ya kuzuia saratani mbalimbali kwenye miili yetu. Pin-Up: https://legalcasinos.com.ua/pin-up-kazino-s-vyvodom-deneg/

Nyama nyeupe ni nzuri sana kama ikitumika kama sehemu ya diet au lishe kwa ajili ya kupunguza uzani kwani ni laini na mwili unaimeng’enya kirahisi sana.

Samaki huwa na vimelea ambavyo ni muhimu sana kwa ajli ya kuzuia tatizo la kusahau sana uzeeni ambalo tafiti zimeonyesha kwamba nyama nyekundu huchangia kwa tatizo hili.

Kiasi cha phosphorus kipatikanacho kwenye samaki ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia macho yaendelee kuona vizuri.

Nyama nyeupe inaweka au husaidia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini katika hali nzuri sana na inaweza kuwafaa sana wagonjwa wa kisukari.

Nyama hii haikai sana tumboni ukilinganisha na mayai hivyo huweza kuzuia tatizo la saratani ya utumbo ambalo ni kubwa sana kwa watumiaji wa nyama nyekundu.