Makala

SIHA NA LISHE: Pilipili mboga na faida zake mwilini

August 20th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

PILIPILI mboga hutumika kama kiungo kwenye mboga za aina mbalimbali nyumbani.

Pengine wasichokijua watumiaji nivirutubisho gani hupatikana ndani yake na kina umuhimu gani kwenye mwili wa binadamu.

Wengi wetu tunaitumia kama kiungo cha mboga na wengine hutumia katika kutengeneza kachumbari ili kuleta ladha na pengine kuipamba kachumbari ionekane ya kupendeza na kuvutia.

Pilipili hoho siyo kali,chungu wala haiwashi,hutofautiana katika ukubwa inategemeana na aina zake.Hupatikana katika mwonekano wa rangi tofauti tofauti,kuna nyekundu, kijani, na njano.

Pilipili mboga husadikika kuongeza virutubisho vya aina ya zeaxanthin na lutein. Haya ni madini ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la kuharibu jicho; ugonjwa ambao hutokea pale ambapo lenzi ya jicho inakuwa na uwingu.

Pia huongeza kinga ya mwili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo kama vile presha ya kupanda na kushuka.

Kwa kula pilipili mboga, utakuwa umeusaidia mwili kuchuja takamwili na pia kutibu muwasho wa vidonda vya kooni.

Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kupunguza shinikizo la damu na kuongeza kiwango cha damu mwilini.

Pilipili mboga zina vitamini C kwa wingi, hivyo husaidia kutibu ugonjwa wa kutokwa na damu puani na kuimarisha kinga ya mwili na kukinga dhidi ya saratani ya kibofu cha mkojo.

Huzuia na kuondoa gesi tumboni; hasa kwa wale wenye tatizo la kuvimbiwa na gesi kujaa.

Wataalamu wa lishe wamethibitisha kuwa pilipili mboga husaidia kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini hivyo huweza kupunguzo uzani.