• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:12 PM
SIHA NA LISHE: Ulaji wa nyama nyekundu una madhara kadhaa mwilini mwa binadamu

SIHA NA LISHE: Ulaji wa nyama nyekundu una madhara kadhaa mwilini mwa binadamu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Kuna nyama nyekundu na nyama nyeupe.

Nyama nyekundu ni ile ambayo ina rangi nyekundu kabla ya kupikwa kama ya ng’ombe, mbuzi na wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne.

Nyama nyeupe ni ilea mbayo ina rangi nyeupe kabla ya kupikwa; mfano kuku, bata, samaki, mbuni na ndege wote wanaotembea kwa miguu miwili.

Hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Nyama ina lehemu.Hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri. Inaweza kusababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi.

Hatari ya kupataugonjwa wa alzheirs

Huu niugonjwawaakiliambaohuwapatawatuwengiuzeeninadaliliyakeikiwanikupotezakumbukumbukabisa. Wanasayansiwanaaminiprotiniinayopatikanakwenyenyamakwajina beta-amyloid huharibumishipayafahamuyakwenyeubongonakuchangiakwaugonjwahuu.

Kifafa

Minyoo inayopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama Taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho. Hali hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.

Unene

Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambayo watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe. Unene na kitambi ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.

Nyama tunazo kula siku hizi sio nyama halisi tena

Ukiangalia nyama a kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotelini, zinakuzwa na kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji.

Magonjwa ya wanyama husika

Miaka ya sasa dunia imekuwa inakumbwa sana na magonjwa ambayo yanashambulia wanyama. Yameua watu wengi na mengine hayatibiki kabisa. mfano; homa ya ndege.

Nyama nyeupe yaani samaki, kuku, bata na ndege wengine wanaoruhusiwa kuliwa ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama ya mbuzi na ya ng’ombe. Na kama wewe tayari una tazizo la moyo, presha, kisukari na kansa, huu ni wakati sahihi wa kuacha kabisa kula nyama nyekundu.

You can share this post!

Kenya Lionesses roho juu baada ya idadi ya washiriki wa...

Mswada wa kuboresha kilimo cha majanichai washabikiwa na...