• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Tanzania mbioni kuunda sheria ya kufungia nje wageni ajira za benki

Tanzania mbioni kuunda sheria ya kufungia nje wageni ajira za benki

NA MWANGI MUIRURI

BENKI Kuu ya Tanzania inalenga kupiga marufuku ajira ya watu wengi kutoka mataifa ya kigeni, wakiwemo Wakenya katika sekta ya kifedha nchini humo.

Iwapo sheria hiyo kielelezo ambayo kwa sasa inajadiliwa itapitishwa, taifa hilo sasa litakuwa likiajiri wageni wasiozidi watano katika kila taasisi za kutoa huduma za kifedha.

Wataalamu wamehoji kwamba Tanzania ina utoshelevu wa akili za kujihudumia katika sekta hiyo.

Aidha, maswali yameibuka kuhusu taifa hilo la Rais Samia Suluhu na kujituma katika kuafikia malengo ya Jumuia ya Afrika Mashariki ambapo nafasi za kiuchumi zinafaa kugawanywa pasipo vizingiti.

Katika sheria hizo mpya Non-Deposit Taking Microfinance Service Providers Regulations, 2024 Watanzania wanafaa kumiliki nafasi za ajira katika sekta hiyo kwa asilimia 95.

Ukitaka kuzidisha kiwango hicho, ni lazima utafute idhini kupitia barua rasmi kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Ili upewe ruhusa ya kukiuka sheria hiyo, ni lazima utoe ushahidi kwamba huduma unazosaka haziwezi zikatolewa na Mtanzania, ama wageni katika ajira hiyo wamekuja kuwapa wenyeji ufundi wa kitaaluma na kuwanoa bongo ili wao wenyewe wajihudumie katika siku za usoni.

Sheria hiyo inaonekana kuzima majirani wa Tanzania hasa Kenya ambao huingia katika taifa hilo na kuanza biashara ya kukopesha wenyeji.

Sasa inaonekana taifa hilo linalenga kutwaa nafasi nyingi za kazi kutoka kwa wawekezaji wa kigeni hasa katika masuala ya kiuchumi.

Jumuia ya Afrika Mashariki hukemea masuala ya ubaguzi katika masoko ya kiuchumi katika mataifa wanachama.

Licha ya kuwa kila taifa mwanachama liko na uhuru wa kujipanga katika kuafikia malengo yake ya kiutawala kwa mujibu wa mkataba na raia wake, sheria zinazoonyesha waziwazi ubaguzi huibua upinzani.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Chama cha wanaume chazua gumzo Meru

‘Vipepeo weupe waashiria dalili za mwaka wa baraka’

T L