• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 12:03 PM
Tanzania yaongoza Afrika Mashariki kwa idadi kubwa ya watu walio na HIV, ripoti yaonyesha

Tanzania yaongoza Afrika Mashariki kwa idadi kubwa ya watu walio na HIV, ripoti yaonyesha

NA WANDERI KAMAU

TANZANIA ndilo taifa linaloongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walio na virusi vya Ukimwi (HIV), imeonyesha ripoti iliyotolewa Alhamisi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Ukimwi (UNAIDS).

Ripoti hiyo ilionyesha Tanzania inaongoza kwa kuwa na watu 1.7 milioni, huku ikifuatwa kwa ukaribu na Kenya na Uganda mtawalia.

Kenya na Uganda zina watu 1.4 milioni kila mmoja wanaoishi na virusi hivyo.

Duniani kote, Tanzania iliorodheshwa katika nafasi ya nne, huku Kenya na Uganda zikiorodheshwa katika nafasi za saba na nane mtawalia.

Afrika Kusini ndilo taifa linaloongoza duniani kwa kuwa na watu wengi zaidi wanaoishi na virusi hivyo duniani. Nchi hiyo ina jumla ya watu 7.8 milioni wanaoishi kwa virusi vya HIV.

Nchi nyingine zinazofuata ni India (watu 2.3 milioni), Msumbiji (2.1 milioni), Nigeria (1.7 milioni) na Zambia, ikiwa na watu 1.5 milioni wanaoishi na virusi hivyo.

Mwaka uliopita, serikali ilisema, licha ya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yaliyo na idadi kubwa ya watu wanaoishi kwa virusi hivyo, asilimia 96 wamekuwa wakitumia dawa za kupunguza makali yake (ARVs).

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizana (NSDCC) mwaka uliopita, jumla ya watoto 7,869 wa kati ya umri wa miaka sufuri na minne wanaishi na virusi hivyo.

Kulingana na takwimu za serikali, kulikuwa na jumla ya maambukizi 22,154 kote nchini mwaka uliopita.

Kati ya maambukizi hayo, 4, 474 ni ya watoto walio kati ya umri wa miaka sufuri na 14.

Kijinsia, wanawake 12,558  na wanaume 5,122 waliambukizwa mtawalia.

Kaunti ya Kisumu ndiyo iliyootajwa kuwa na watu wengi wanaoishi na virusi hivyo, ikifuatiwa na Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi ahadi hewa za wanasiasa na mwingilio wa makateli...

Muriu, Njuguna na Wasary waongoza ukaidi dhidi ya ushuru wa...

T L