• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Kiini cha makosa katika lugha

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Kiini cha makosa katika lugha

Na MARY WANGARI

Tatizo la Msamiati

HALI hii hutokea kwa sababu ya ugeni wa dhana au fikra katika lugha ya Kiswahili. Kwa mfano:

Kuora badala ya kuondoka

Nitakula mchele badala ya Nitakula wali

Amepeleka dada yangu badala ya Amemwoa dada yangu

Watu wasita badala ya Watu sita.

 

Makosa ya Kimakusudi

Makundi ya wanasarakasi na machale hutokeza na makosa katika matumizi ya lugha ili kuwatumbuiza watu.

Wasanii mathalan huiga watu maarufu na hasa wanaofanya makosa ya lugha ama kutokana na athari za lugha ya mama au sababu nyinginezo.

 

Hali ya kiakili wakati mtu anatumia lugha

Mtu aliyevurugika akili, kwa mfano, kutokana na vileo, huwa hana utawala wa mkondo wa akili na ulimi ambao ni muhimu katika lugha.

Hivyo, huwa na makosa mengi ya kisarufi katika matamshi. Vivyo hivyo, mtu aliyechoka kiakili hufanya makosa ya lugha.

 

Kutoelewa kanuni za matumizi ya lugha

Matumizi ya lugha hudhibitiwa na kaida fulani ambazo zikikiukwa, makosaya kimatumizi hutokeza.

Kwa mfano, maamkizi katika Kiswahili, mkubwa kiumri hawezi kumwamkua mdogo shikamoo! Siku zote mdogo humwamkua mkubwa hivyo.

Hata hivyo, baadhi ya watu wakubwa aghalabu husikika wakiwaamkia wadogo Shikamoo. Hili ni kosa.

 

Ujumuishaji wa kanuni za kisarufi

Ujumuishaji wa kanuni zinaotawala sarufi katika muktadha mmoja piahusababisha makosa katika lugha. Kwa mfano, katika mnyambuliko wa vitenzi, ujumuishaji wa kanuni za unyambuaji katika muktadha moja huchangia kuweko kwa makosa mengi katika matumizi ya lugha.

Vitenzi vingi vinaponyambuliwa katika kauli ya kutendesha, viishio huwa ni –esh-a. Hili huwafanya wengi kufikiria kuwa kanuni hii ni ya kipekee na kuwa kila kitenzi kinaponyambuliwakatika kauli hii huishia kwa –esh-a.  Kwa hivyo,kila kitenzi hulaimishwa kuchukua kiishio hicho, -esh-a, ilhali sivyo.

Kuna vingine ambavyo huchukua kiishio -z-a. Mifano:

Kosa                                                Sahihi

Kimbisha                                            Kimbiza

Pungusha                                           Punguza

Ungusha                                             Unguza

Chukisha                                            Chukiza

 

Makosa ya kimantiki

Kukosa mtiririko wa fikra huweza kuzua upotevu wa mawazo. Kwa mfano:

Nyasi ya kijani ndani ya nyoka badala ya Nyoka wa kijani ndani ya nyasi.

 

[email protected]

Marejeo

Chiraghdin, S. & Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.

Richards, J.C. (1984). Error Analysis Perspectives on Second Language Acquisition. London: Longman Group Ltd.

Wardhaugh, R. (1986). An Introduction to Socio-Linguistics. New York: Blackwell Publisher.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Kiini cha makosa katika lugha

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Kuzungumza au kuwaza kwa haraka...

adminleo