• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:50 AM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Lahaja

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Lahaja

Na MARY WANGARI

LAHAJA YA KIBARAWA

HII ni lahaja inayotumiwa na wazungumzaji wa Kiswahili katika eneo la katikati ya Mogadishu, Somalia. Lahaja hii huzungumzwa katika maeneoya Marka na Barawa, si ajabu baadhi ya wataalamu huizungumzia kama lahaja ya Kibarawa.

Kwa Mfano:

CHIMINI/ KIBARAWA KISWAHILI SANIFU
oloka Ondoka, nenda
Milu Miguu
Chintu kitu
Shikilo sikio
ikulu kubwa, tukufu

LAHAJA ZA KATI

KIMVITA

Hii ni lahaja inayozungumzwa katika kisiwa cha Mombasa au Mvita kama ilivyojulikana zamani. Lahaja hii ina sifa zinazokaribiana sana na za Kiamu.

Katika lahaja ya Kimvita, sauti ‘t’ inachukua nafasi ya sauti‘ch’ katika Kiswahili sanifu.

Kwa mfano:

KIMVITA KISWAHILI SANIFU
mtele mchele
mtuzi mchuzi
mwivi mwizi
vyaa zaa
mtanga mchanga

KIJOMVU/CHIJOMVU

Ni lahaja ambayo hutumiwa katika maeneo ya pembeni ya mji waMombasa, kaskazini nje ya kisiwa cha Mombasa.

Katika lahaja hii, maneno ambayo katika Kiswahili sanifu huanza kwa sauti ‘ki’ hubadilikana kuwa ‘chi’.

Kwa mfano:

KIJOMVU KISWAHILI SANIFU
Chiyana kijana
chichi hiki
chioo kioo
chamba kwamba
wenjine wengine

KINGARE

Ni lahaja inayosemwa Mombasa katika maeneo ya kiwanja cha ndege na Kilindini.

Kwa mfano:

KINGARE KISWAHILI SANIFU
nzee mzee
yakwe yako
geshi jeshi

LAHAJA ZA KUSINI

KIVUMBA

Hii ni lahaja ya Kiswahili ambayo huzungumzwa katika sehemu za Vangana Wasini (sehemu za kusini mwa Mombasa). Lahaja hii inaonyesha matumizi ya sauti ‘r’ badala ya ‘t’ katika Kiswahili sanifu.

Kwa mfano:

KIVUMBA KISWAHILI SANIFU
kuogova kuogopa
ngia njia
mroro mtoto
vira pita
rosini sote

CHICHIFUNDI/CHIFUNDI

Hii ni lahaja inayozungumzwa Shimoni au kaskazini mwa Vanga, kusini mwa pwani ya Kenya.

CHICHIFUNDI KISWAHILI SANIFU
vochea pokea
kadzi kazi
njisi ngisi
sichia sikia

KIMTANG’ATA

Hii ni lahaja inayozungumzwa katika eneo la pwani ya Mrima, Pangani na hata Tanga.

Ni lahaja inayoonyesha uhusiano wa karibu sana na lahaja ya Kimvita na Kijomvu.

Kwa mfano:

KIMTANG’ATA KISWAHILI SANIFU
oka choma
munyu chumvi
Fyoma soma
chama hama

[email protected]

Marejeo

Chiraghdin, S., & Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.

Richards, J.C., (1984). Error Analysis Perspectives on Second Language Acquisition. London: Longman Group Ltd.

Wardhaugh, R. (1986). An Introduction to Socio-Linguistics: New York: Blackwell Publishers.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Lahaja za Kiswahili na maeneo...

Gavana Waititu aonya matapeli wanaohangaisha watumiaji wa...

adminleo