• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 5:55 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nadharia ya Mawasiliano ya Kiutambulisho

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nadharia ya Mawasiliano ya Kiutambulisho

Na MARY WANGARI

Jane Rocky aliuliza hivi: Eleza uhusiano wa lugha na jamii kwa kutumia nadharia ya makutano na mwachano ya Giles

Nadharia ya Mawasiliano ya Kiutambulisho

NADHARIA hii iliasisiwa na mwanaisimu Giles (1972 & 1982).

Nadharia hii inarejelea dhana ya utambulisho kama kigezo maalumu kinachotumiwa kumtambulisha mtu, kundi la watu, jamii au taifa fulani.

Kwa mujibu wa nadharia hii, utambulisho huwa na vibainishi muhimu vinavyojumuisha lugha, mahali, uchumi, utamaduni, siasa, mavazi, na chakula. Haya yote hutumiwa kuukamilisha utambulisho.

Viambajengo muhimu vya nadharia ya utambulisho

Nadharia ya utambulisho inasheheni mawazo makuu jinsi tulivyoyaainisha ifuatavyo:

1. Huhusika na mahusiano kati ya lugha, muktadha na utambulisho.

2. Nadharia hii huangazia kuwa watu wanapoingiliana wanabadilishana usemi, sauti na hata ishara ili kujihusisha na wengine kwa mujibu wa Turner na Richard (2010)

3. Hutalii sababu ambazo huwafanya watu kusisitiza kupunguza tofauti kati yao wakati wa mazungumzo. Huangazia sifa za kibinafsi na za makundi ambazo husababisha ujihusishaji na pia huchunguza namna mamlaka, miktadha ya kimaikro na kimakro huadhiri tabia za mawasiliano.

4. Huchukulia kuwa watu huingiza tamaduni na tajriba katika maingiliano kupitia kwa mazungumzo na tabia. Hivyo basi usemaji na tabia za kufanana hutawala katika mazungumzo.

5. Husadiki kuwa ujihusishaji huathiriwa na jinsi watu huchukulia na kuthamini yale ambayo huendelea wakati wa mazungumzo; kumaanisha namna watu hutafsiri na kuhukumu jumbe katika mazungumzo

Dhana ya utambulisho

Dhana ya utambulisho ni pana mno kwa kuwa inafumbata mambo mengi ndani yake.

Kwa muhtasari, utambulisho ni jumla ya vigezo maalumu vinavyotumiwa kumtambulisha mtu, kundi la watu, jamii au taifa fulani.

Vigezo hivi hubainisha kuwa kundi fulani ni tofauti na lingine, jamii moja ni tofauti na nyingine, mtu mmoja ni tofauti na mwingine au taifa moja kuwa tofauti na lingine.

Kihore na wenzake (2009), wanasema vigezo ambavyo hubainisha utambulisho wa mtu au jamii vinaitwa vibainishi. Vibainishi hivi vinahusisha:

i. lugha

ii. utamaduni

iii. historia ya jamii

iv. siasa

v. uchumi

vi. dini

vii. mavazi na kadhalika

 

[email protected]

Marejeo

Adegbija, E. (1999). “Titbits on Discourse Analysis and Pragmatics” in the English and Literature in English. An Introduction . Unilovin: Department of Modern European Languages, Unilovin.

Anderson, J. A & Meyer, T.P (1988). Mediated Communication: A Social interaction perspective. Newsbury Park, CA: Sage

Askew, K. (2003). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics. Dar es Salaam: Kapsel

  • Tags

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Utayarishaji wa mitihani katika...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Chimbuko la Nadharia ya...

adminleo