UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya lugha sanifu katika jamii
Na MARY WANGARI
LUGHA sanifu ni iliyosanifishwa kimatamshi, kisarufi, kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi.
Aidha, ni lugha iliyowekewa kanuni zinazotawala jinsi maneno yanavyondelezwa pamoja na msamiati.
Lugha sanifu inasheheni sifa zifuatazo:
- Husanifishwa na serikali kama sera ya lugha.
- Aghalabu huwa ni lahaja iliyoenea zaidi kuliko nyingine.
- Huwa na msamiati mpana.
- Huweza kukubali msamiati mpya kama vile wa kiteknolojia.
- Huunganisha watu katika kutekeleza shughuli za kijamii na kitaifa.
- Ndiyo inatumika shuleni na hata katika uchapishaji wa vitabu.
- Hutumika katika kutafsiri maandishi maalumu kama vitabu vitakatifu.
Dhima na umuhimu wa Lugha Sanifu katika jamii
Lugha sanifu hutekeleza majukumu yafuatayo katika jamii:
Husawazisha matumizi ya lugha kimaendelezo (tahajia), kimatamshi,kimaandishi, kimsamiati na kisintaksia.
Husawazisha matumizi ya lugha kimaendelezo (tahajia), kimatamshi, kimaandishi, kimsamiati na kisintaksia.
Hutumika katika mafunzo shuleni.
Hutumiwa kuchapisha vitabu.
Hutumika kuandika sera za serikali na kuzisambaza.
Hutumika katika uandishi wa magazeti, majarida, mabango na kadhalika.
Hutumika katika mijadala katika mikutano ya kitaifa na kimataifa.
Hutumika katika kuandika barua rasmi, Katiba ya nchi, hati na stakabadhi nyinginezo rasmi.
Hutumika katika kutafsiri maandishi maalumu kama vile vitabu vitakatifu.