• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Sajili katika miktadha isiyo rasmi

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Sajili katika miktadha isiyo rasmi

Na MARY WANGARI

MIKTADHA isiyo rasmi ni ile ambayo wazungumzaji huwa na uhuru wa kutumia lugha bila kubanwa na kanuni za kisarufi na kaida nyinginezo.

Mifano ya miktadha hii ni kama vile nyumbani, dukani, sokoni na kadhalika.

Mazungumzo ya kawaida

Haya ni mawasiliano au mazungumzo ya ana kwa ana. Mazungumzo haya yanaweza yakatokea katika miktadha kama nyumbani, mitaani au barabarani. Nayo yana sifa zifuatazo:

Ucheshi na utani – Lugha inayotumiwa husheheni utani na ucheshi kwa sababu ya kutokuwepo kwa matarajio ya urasmi, mzungumzaji au wazungumzaji wana uhuru mkubwa zaidi katika matumizi ya lugha.

Matumizi ya sentensi fupifupi – Sentensi zinaweza kukatwakatwa ili kurahisisha kueleweka kwa msemaji.

Matumizi ya sentensi fupifupi husababishwa na mambo mbalimbali kama uwezekano wa anayezungumza kuyakatiza anayoyasema kwa sababu ya kupotelewa na yale aliyokusudia kuyasema. Aidha, inaweza kutokana na tabia ya wazungumzaji kukatizana mazungumzo.

[email protected]

Marejeo

Massamba, D.P.B. (2002). Historia ya Kiswahili 50 BK. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ipara, I. O. & Waititu, F.G. (2006). Ijaribu na Uikarabati. Nairobi: Oxford University Press.

Habwe, J. (2006). Darubini ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Maddo, U. & Thiong’o, D. (2006). Mazoezi na Udurusu: Kiswahili 102/2. Nairobi: Global Publisher.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Sababu za kuchanganya au...

Moto: Wafanyakazi wa juakali wakadiria hasara Viwandani

adminleo