• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vitengo vya Semiotiki

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vitengo vya Semiotiki

Na MARY WANGARI

KIELEKEZI – Kulingana na Peirce, kielekezi hueleza na kufafanua uhusiano uliopo baina ya ishara na kinachoashiriwa.

Kwa mfano katika kazi ya fasihi, kunaweza tokea kilio katika giza na kuashiria kuwepo kwa mtu fulani.

Ishara-tanakali – Kitengo hiki huonyesha mahali au hali ambapo pana uhusiano kati ya ishara na kiashiriwa.

Katika kipengele hiki, michoro au picha ni ishara- tanakali zinazoeleweka. Kwa mfano milio,‘miaoo’ ni ishara – tanakali au sauti ya paka.

Taashira – Pierce anagusia dhana ya taashira ambayo aliitumia kuelezea aina ya ishara inayoashiria kutegemea matumizi ya kinasibu na kikawaida au ya kidhahania.

Anadai kuwa ishara hutegemezwa kwenye msingi fulani ili kufasiriwa na hili linaoana na dai la Mswisi Saussure kuwa ishara hazina upekee wa maana ila zinapofasiriwa.

Kupitia juhudi zake, nadharia ya semiotiki haikuishia kuzisambaza sifa za kitaaluma sana kama ulivyofanya umuundo.

Hata hivyo, Wafula na Njogu wamedhihirisha kwamba Mswizi katika uchanganuzi wake wa kisemiotiki, alijikita sana katika dhima ya ishara katika jamii naye Peirce akatafiti namna ishara zilivyotumiwa kufafanua vitendo maalumu na maana ya ishara hiyo ikitokana na sheria fulani za kiutamaduni, kitanzu na lugha.

Baruapepe ya mwandishi: [email protected]

Marejeo

Mulokozi, Mugyabuso & Kahigi K.(1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing                   House.

Njogu, K. & R.M. Wafula (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Shihabuddin, C. (1970). Utangulizi. Malenga wa Mvita. Nairobi: Oxford University Press

You can share this post!

Ajali baina ya gari la pesa, basi yaua watano

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nadharia ya Simulizi/ Naratolojia

adminleo