• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
UKUZAJI MBOGA: Maarifa yanayohitajika katika kukuza kabichi zenye faida kwa mkulima

UKUZAJI MBOGA: Maarifa yanayohitajika katika kukuza kabichi zenye faida kwa mkulima

Na GRACE KARANJA

KABICHI hukuzwa na wakulima wa ngazi zote; wakulima wadogowadogo pamoja na wale wanaolima katika mashamba makubwa.

Katika Afrika Mashariki, zao hili hukuzwa Kenya, Uganda na Tanzania.

Hapa Kenya kabichi hukuzwa katika maeneo yaliyo na baridi na unyevunyevu hivyo basi wakulima walio na vitovu vya maji wamekuwa wakijikakamua kwa njia zote kuhakikisha pia wao wanaendeleza kilimo cha aina hii ya mboga.

Kabichi huwekwa katika makundi mawili, zile za vichwa vidogo na vya wastani ambazo hufaa soko wazi na zile ambazo zina vichwa vikubwa ambazo huliwa sana katika shule, hospitali na hoteli.

Kulingana na mtaalam wa mbegu kutoka kampuni ya Starke Aryes kwa ujumla kabichi hustawi karibu kwenye udongo wa aina zote; kuanzia udongo wa kichanga laini hadi udongo wa mfinyanzi.

Hata hivyo anasema kupima mchanga kabla ya kuanzisha kilimo ni muhimu ili kufahamu madini yanayopungua katika udongo .

“Wakulima kutoka maeneo tofauti nchini wanaweza kulima mboga hii bila kuchagua aina ya udongo. Inafanya vyema katika udongo wa kichanga laini ambapo hutoa mazao mengi na kabichi zenye uzito mkubwa ukifuatiwa na mfinyanzi. Udongo wenye tindikali nyingi huzorotesha ukuaji wa kabichi. Udongo mzuri kwa kabichi ni ule ulio na tindikali kati ya ph 5.5 – 6.5,” anaeleza mtaalam wa mbegu kutoka kampuni ya Starke Aryes tawi la Kiambu.

Hata hivyo, mtaalamu huyu anahimiza wakulima wa kabijchi kuzingatia yafuatayo ili kufanya kilimo biashara kilicho na faida. Kwanza anatahatharisha wakulima kutembelea wataalam na kujua aina ya kabichi inayo fanya vizuri katika maeneo waliyoko.

Pili mashamba yaliyo na udongo wenye rutuba ya kutosha hasa yaliyo na naitrojeni pamoja na phosphorous yatafaa zaidi.

Anasema kuwa mbolea aina ya samadi iliyooza vizuri huongeza ukuaji wa haraka na ubora wa kabichi kuliko mbolea za viwandani.

Mtaalam huyu anasema kupanda mbegu katika kitalu kilichoinuka husaidia mbegu kutobebwa na maji wakati wa umwagiliaji au mvua kubwa. Matandazo yaondolewe mara baada ya mbegu kuota. Punguza kiwango cha kumwagilia maji siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, kati ya siku 6 – 12,” anaeleza.

Jinsi ya kupanda kabichi

Kabla ya kupanda mimea ya kabichi shamba litayarishwe vizuri na kuchimbwa mitaro kabla ya mwezi mmoja au miwili ili kuhamishia mimea.

Makoongo; yaani mashimo yawe sentimita 45 kutoka katikati mwa shimo moja hadi lingine huku mbolea ikiwekwa kiasi cha mkono kwa kila shimo.

Kuna umuhimu wa kusitisha umwagiliaji maji mimea kati ya siku nne hadi sita ili kuipa uzoefu wa hali geni katika shamba la kuhamishia.

Kitalu Mashimo yamwagiliwe maji masaa machache ili wakati wa kung’oa miche kabla ya mimea kupandikizwa.

Miche iliyo na afya nzuri, mizizi yenye afya, iliyo na majani kati ya 3 – 5, ioteshwe siku hiyo iliyong’olewa wakati wa jioni.

Miche ing’olewe pamoja na udongo wake na kupandwa kimo kile kile kilichokuwa kitaluni.

Maji yamwagiliwe punde tu baada ya kupandwa. Ikiwa mkulima anatumia mbolea kutoka viwandani basi kipimo kinachofaa cha gramu 10 yaani kijiko kidogo cha chai kichangawe kwa mchanga na mbolea ya mifugo iliyooza.

You can share this post!

Dai vigogo Real Madrid hawana makali tena

Nguvu mpya za Raila serikalini

adminleo