Makala

ULIMBWENDE: Jinsi ambavyo unaweza kutunza nywele zako

March 5th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na MARGARET MAINA

[email protected]

WANAWAKE wengi wa Kiafrika husuka nywele zao kwa mitindo mbalimbali. Hii ina maana kwamba urembo wa kusuka nywele ni wa aina au jinsi mbalimbali.

Aina nyingine ni rahisi kutengeneza huku baadhi ikiwa ni ngumu ambapo inakuhitaji muda mrefu kuzitengeneza nywele.

Mitindo rahisi kama vile kuchana na kubana nywele huchukua muda usiozidi nusu saa wakati mitindo migumu kama rasta ndogo na nyembamba ikiweza hata kuchukua muda wa saa 5 hadi 8 kama unashughulikiwa na msusi mmoja.

Bei ya usukaji pia hutofautiana kulingana na ugumu wa mtindo na muda unaotumika.

Kunyoa kipara

Wapo wanawake wengi wanautumia mtindo huu wa kunyoa na wanapendeza.

Nywele fupi za kuchana au kusuka

Mtindo huu ni rahisi na pia unaweza kufanya mwenyewe nyumbani na ni wa haraka na hauhitaji pesa.

Nywele ndefu za kubana

Mtindo mwingine rahisi ni kuchana na kubana katika namna tofauti. Unaweza ukatumia vibanio vya nywele au ukazifunga kwa kitambaa.

Nywele zinatakiwa kupumzika kidogo baada ya kusukwa katika mitindo ya kubana sana.

Selfie ya Margaret Maina akiwa amezichana nywele zake. Picha/ Margaret Maina

Kutengeneza nywele

Mitindo hii ni migumu, huchukua muda mrefu na hivyo ina bei za juu kusuka.

1. Rasta za bandia

Mtindo huu hukuhitaji kutumia nywele bandia kusuka na ni mzuri na hufanya wanawake wengi wawe wa kupendeza.

2. Rasta za asili

Hizi, mrembo hahitaji kutumia nywele za kuongeza. Nywele asili husokotwa katika mafungu madogomadogo.

3. Laini (cornrows)

Ni mtindo maarufu na unapendwa na wanawake wengi – wa mashinani na wa mijini.

Tazama picha hizi:

Selfie ya Margaret Maina akiwa ametengeneza nywele zake nadhifu. Picha/ Margaret Maina
Margaret Maina akiwa ametengeneza nywele zake. Picha/ Hisani

Chagua mtindo utakaokufaa

Kuna mitindo mingi ya kusuka nywele, mingine ni rahisi na inahitaji muda mfupi wakati mingine ni migumu na inahitaji muda mrefu na ni ya gharama kubwa.

Ukiwa na muda mfupi wa kujiandaa utahitaji mtindo rahisi.

Pia mtindo utakaouchagua ama uwe ni mtindo wa ofisini au kama ni kwa ajili ya safari, unaweza ukatofautiana na ule wa kutengeneza kwa ajili ya sherehe au shughuli nyingine ya kijamii.