ULIMBWENDE: Jinsi unavyoweza kuitunza ngozi ya chini ya macho
Na MARGARET MAINA
NGOZI inayozunguka jicho ni laini zaidi kuliko ngozi ya uso wako wote.
Ngozi hii ni muhimu sana kwani ina ulaini na inahitaji uangalifu mkubwa. Sehemu hii ya ngozi ni nyembamba mno na inaweza kupata madhara na kitu kidogo kabisa pamoja na kwamba inaweza kuzeeka mapema kabla ya muda wake.
La muhimu ni kwamba ni lazima uoshe vitu unavyotumia kuremba jicho lako.Bidhaa nyingi zinazotengenezwa kuondoa vipodozi katika jicho zimetengenezwa katika mazingira ya kuhakikisha kwamba ngozi inabaki hai na isiyokuwa na matatizo.
Inatakiwa kila asubuhi unapoamka asubuhi ni vyema ukaanza na krimu yenye unyevunyevu na unapoenda kulala wakati wa usiku. Kwa kuwa umri unavyozidi kuongezeka ngozi huacha kujirejesha inavyotakiwa na huondoa ule ulaini wake iliokuwa nao kwanza kuhakikisha kwamba eneo hilo lina unyenyevu husaidia kuweka ngozi ile katika hali bora zaidi.
Ni vyema ukahakikisha kwamba moisturizers unayotumia ina SPF(Sun Protecting Factor) kuanzia 30 hadi 50 ili kuhakikisha kwamba ngozi inayozunguka jicho inachungwa vyema dhidi ya mikunjo inayosababishwa na miale ya jua.
Njia nzuri pia ya kupunguza uvimbe wa macho ni kuweka maski kuzunguka jicho.
Pia unaweza kumasaji eneo hili ili kuondoa sumu ambayo imejijenga katika mfumo wa tezi.
Tatizo la mikunjo katika ngozi inaweza kudhibitiwa kwa kutumia bidhaa za urembo zenye asidi ya glycolic ambayo pia hujulikana kama alpha hydroxy acid au AHA.
Kuna njia pia za asilia mbazo zinaweza kusaidia kuweka sawa ngozi inayozunguka jicho kama vipande vya matango.
Unahitaji tango moja kubwa. Kata tango lako kwenye vipande vidogo vya duara, weka kwenye friji vipate baridi kwa dakika 15 ,Kisha weka machoni.
Fanya hivi kila siku mara moja. Ngozi ya jicho lako Itakuwa na afya na utaondoa Weusi wa jicho.
Pia unaweza kutumia mafuta ya mizeituni kuzunguka macho yako kila siku na utaona mabadiliko