ULIMBWENDE: Jinsi ya kutunza ngozi yako msimu huu wa baridi
Na MARGARET MAINA
MSIMU huu wa baridi, changamoto kubwa ni kijibaridi na upepo ambao unasababisha ukavu wa ngozi.
Hali hii kwa wengine inafikia hadi kukatika midomo na miguu na maeneo mengineyo ya mwili.
Unaweza kufanya mambo kadhaa yatakayosaidia kuitunza ngozi yako.
Kunywa maji ya kutosha
Wakati huu aghalabu watu wengi hawana mazoea ya kunywa maji sana kwa sababu ya hali ya kijibaridi ila njia yenye matokeo mazuri ni kujitahidi kunywa maji. Kwenye maji yako pia unaweza kuongeza limau au ununue maji yenye ladha tofauti.
Ongezea Face oil kwenye mafuta yako
Ukimaliza tu kupaka moisturiser yako, jipake face oil ili kufunga unyevu unyevu wako na hutahisi ukavu zaidi.
Wakati huu usi-scrub uso wako zaidi ya mara moja
Wakati wa kipupwe, ngozi inapoteza unyevu kwa urahisi. Ukishindwa ku-moisturise ngozi yako unaandaa mazingira mazuri ya ngozi kukauka na hutajisikia vizuri. Scrub kwa sasa ni ufanye mara moja tu kwa wiki. Usizidishe kwa sababu utasababisha ukavu zaidi.
Na baada ya kumaliza kufanya scrub yako, tumia maski papo hapo uifanyie haki ngozi yako.
Tumia hand creams
Usiache mikono yako ikawa mikavu. Hakikisha unatumia hand cream.
Kwenye lips tumia, Lip balm, na lip jelly.
Tena ikibidi uwe unaweza kuibeba kwenda nayo sehemu mbali mbali. Kwa wewe ambaye una tabia wakati sehemu za mdomo zimekauka unalambisha mate wakati wa kipupwe na baridi kufanya hivi hakutakusaidia. Isitoshe, unaweza kupata vidonda.
Vaa nguo zenye kufunika mwili wako vizuri
Hizi ni nguo ambazo wewe mvaaji utakuwa sawa unapofanya shughuli zako. Kumbuka unapojiacha wazi, upepo ukikupiga utakauka zaidi. Fanya chaguo bora la nguo unazovaa.
Pata muda mzuri wa kupumzika
Na usiache kujipaka mafuta usiku kwa sababu ngozi yako inajitengeneza vizuri usiku. Hasa wakati huu ambao inabidi ufanye kazi ya ziada kujilinda.