• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
ULIMBWENDE: Majani ya giligilani katika urembo

ULIMBWENDE: Majani ya giligilani katika urembo

Na MARGARET MAINA

[email protected]

GILIGILANI ni kiungo cha kawaida sana. Wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi mbalimbali.

Kina harufu nzuri na ladha tamu.

Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.

Giligiliani ina wingi wa Vitamini A, B6, C, B12, pia ina wingi wa madini ya chuma, Calcium na Magnesium.

Giligilani husifika kwa kuwa dawa na kinga ya magonjwa mengi.

Historia inaonyesha kwamba kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu azali nchini Misri.

Ni vyema kujua kwamba kwa kusema chakula fulani ni dawa, basi maana hapa ni kwamba chakula hicho kina virutubisho fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa fulani au kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga dhidi ya ugonjwa fulani.

Giligilani huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi. Mtumiaji anahitaji giligilani kiasi manjano (Binzari Manjano) kiasi cha kijiko kimoja tu.

Ili kuondoa chunusi na madoa meusi, twanga majani ya giligiliani, chuja au kamua ili kupata maji yake.

Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko kimoja cha manjano (Binzari manjano).

Paka kwenye ngozi, kisha acha ikauke kabla ya kusafisha ngozi kwa maji moto.

Onyo: Usisugue ngozi bali paka taratibu.

Huipa ngozi mng’ao. Tafuta giligilani kiasi na tango moja. Saga giligilani na tango pamoja upate mchanganyiko mzito ambao utatumia kama maski. Paka usoni. Baki nayo kwa dakika 20 kisha tumia maji ya kawaida kusafisha. Rudia kufaya hivi kwa wiki kadhaa. Maski hii inatumika kwa ngozi aina zote, lakini ni nzuri zaidi kwa wenye ngozi za mafuta.

You can share this post!

Ukosefu wa fedha za kutosha watatiza utafiti kuhusu...

Wakazi Kambiti walalamika kuhusu ubovu wa barabara

adminleo