Makala

USWAHILINI: Faida kemkem za mafuta ya nazi kwa Wapwani na wabara

July 3rd, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na HAWA ALI

MAFUTA ya nazi ni mojawapo ya bidhaa za asili zenye matumizi yanayoleta matokeo mazuri katika urembo na afya kwa ujumla na hutumiwa sana katika maeneo ya Uswahilini na maeneo mengineyo nchini na hata nje ya nchi.

Ukizingatia kwamba ni mafuta yanayopatikana kirahisi na pia hata yakichujiwa viwandani na kufungashwa bado bei yake ni nafuu sana ukilinganisha na faida zake katika ulimwengu wa urembo.

Yafuatayo ni baadhi ya manufaa ya mafuta ya nazi.

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolestro mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.

Haya ndiyo mafuta yenye uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini.

Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida.

Isitoshe, mafuta ya nazi hung’arisha ngozi.

Sio sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha.

Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji ama kuuchua mwili wako.

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo.

Kwa hiyo, ikiwa unatafuta kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.

Mafuta yenye afya

Mafuta ya nazi ni mafuta mbadala ya kupikia yenye afya.

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya.

Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

Huzuia maradhi mengi hatari mwilini. Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric.

Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibiti na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini.

Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne na utaona maajabu.

Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu: Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).