• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
VIDUBWASHA: Kitakujuza ikiwa mtoto ana maambukizi sikioni (Teslong Wireless Otoscope)

VIDUBWASHA: Kitakujuza ikiwa mtoto ana maambukizi sikioni (Teslong Wireless Otoscope)

Na LEONARD ONYANGO

IKIWA mtoto wako analia mara kwa mara huku akijikuna sikio na hata kushindwa kulala, hiyo ni dalili kwamba ana maambukizi katika sikio.

Wataalamu wanasema kuwa mtoto aliye na maambukizi ndani ya masikio huwa na maumivu ya kichwa na hata kushindwa kula.

Lakini dalili hizo huenda zikawa za ugonjwa tofauti.

Simu yako sasa inaweza kukusaidia kuwa na hakika ikiwa kweli mtoto anasumbuliwa na maambukizi au kitu kimeingia ndani ya sikio lake.

Kifaa cha Teslong huunganishwa na simu na kisha kuwekwa ndani ya sikio la mwathiriwa.

Hunasa picha na kuzionyesha katika skrini ya simu.

Ikiwa hujui chochote kuhusu sikio, unaweza kumtumia daktari picha hizo na akakueleza kinachosumbua mtoto.

Kifaa hiki kinaingiliana na simu za Android, iPhone na kadhalika.

Kuchokonoa kwaweza kuwa ni hatari

Wataalamu wanashauri kuwa kitu au mdudu anapoingia ndani ya sikio, usianze kuchokonoa kwa kijiti au kifaa chochote kwani huenda ukakisukuma ndani zaidi.

Inamisha kichwa upande wa sikio lililoathirika. Kwa kufanya hivyo unaongeza uwezekano wa kitu hicho kutoka chenyewe.

Ikiwa ni mdudu, wataalamu wanashauri umimine mafuta kidogo ya uvuguvugu kumwezesha kutoka mwenyewe.

You can share this post!

TEKNOHAMA: Hatua kubwa katika matibabu ya ubongo

VIDUBWASHA: Kitaepusha maafa zaidi wakati wa tetemeko la...

adminleo