Vijana 56,000 kufaidika na mkopo wa Sh800,000 kila vijana wawili
NA KEVIN ROTICH
Huku Kenya ikikabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, serikali na mashirika ya kibinafsi imeanza mchakato wa kuwekeza katika sekta ya kilimo, ujenzi na viwanda ili kubuni nafasi zaidi za kazi.
Ukosefu wa kazi umesababisha idadi kubwa ya vijana kujitumbukiza kwenye lindi la mihadarati, ukahaba na uhalifu.
Ni kutokana na haya ambapo mashirka ya KCB na Mastercard Foundation yamewekeza kima cha Sh34.4 bilioni katika mradi wa vyumba vya mvungulio (greenhouses) kote nchini.
Ufadhili wa Sh21.6 bilioni unatoka katika benki ya KCB ilhali Sh12.5 bilioni ni kutoka kwa Mastercard Foundation.
Mkurugenzi mkuu wa KCB Foundation Jane Mwangi amesema vijana 56,000 katika maeneo 560 kote nchini watafaidika na mkopo wa Sh800, 000 kwa kila vijana wawili.
“Benki itawapa vijana hao muda wa miezi sita kabla ya kuanza kulipa mikopo hiyo na jumla ya miezi kumi na mbili kulipa madeni,” Bi Mwangi anasema.
Mkopo huo wa 800, 000 utatumika katika kuunda, kusimamia mahitaji kama umeme, ulinzi na mfanyikazi kwa mwaka mzima.
Hata hivyo, Bi Mwangi anasema kuwa mkopo huo bado hautoshi kwani kila mradi unahitaji kima cha Sh1, 200, 000.
“Sh400, 000 za ziada ni za kuchimba kidimbwi cha maji, kuweka kawi ya jua, na kulipa wenye miradi mishahara,” anaongezea.
“Kwa nafasi za ajira milioni moja unusu ambazo mradi huo unatarajia kuunda kote nchini, 1, 300, 000 zitatokana na ukulima, elfu 100, 007 kwa viwanda na 116, 000 katika ujenzi,” anasema.
Baadhi ya mazao yatakayopandwa ni kama vile yyanya, dania, pilipili hoho na mboga.
Bi Mwangi anasema kila mradi utasimamiwa na vijana wawili na mfanyikazi mmoja. Pia, watawapa mafunzo zaidi ya vijana 63,000 kwenye vyumba vya mvungulio ilhali 56,000 watapokea mikopo.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya KCB Joshua Oigara anasema wahusika watasaidiwa katika kuuza mazao yao.
“Pia tutawapa mawaidha ya hali ya juu kwa jinsi ya kuendeleza miradi yao kutoka kwa wataalamu wa masoko,” Mr Oigara said.
Bwana Oigara anasema mradi huo ndio mkubwa zaidi barani Afrika kwa uwekezaji baina yao na MasterCard Foundation.
Alisema kuwa kilimo kinapaswa kutamalaki mfumo mpya wa teknolojia kutoka mbinu za zamani.
“Tatizo kubwa la wakulima wengi ni kupanda mimea bila kuzingatia watakapouza mazao yao,” Oigara anaongezea huku akisema wakulima wengi wanaofanya kazi kwa masaa marefu hawapokei mazao mengi.
Anasema sekta ya kilimo ni nguzo muhimu katika harakati za kuunda nafasi za kazi milioni 11 hadi milioni 15 kwa kila mradi.
“Vijana wataweza kupokea mapato sawa yatakayowawezesha kununua vyumba vya biashara,” anasema.
Walikuwa wakizungumza walipozindua mradi wa kwanza wa vyumba vya mvungulio mia moja katika eneo la Ngong, katika Jimbo la Kajiado.
Maeneo yatakayofuata kwenye mradi huo ni Limuru, Ongata Rongai na Juja.
Waziri wa Kilimo Peter Munya anasema wizara yake itashiriakiana na mradi huo ili kuhakikisha imetekelezwa ipasavyo.
“Yangu ni kuwahakikishia kwamba Wizara ingependa kushirikiana nanyi ili mradi huu ufaulu. Pia, tuko karibu kuzindua mradi mwingine kama huu hivi karibu na tungependa kushirikiana,” Waziri Munya anasema.
Waziri Munya anaongeza kuwa serikali itatoa mkopo wa Sh800 milioni ili kukuza mradi huo.
Kila mradi unatarajiwa kuchukua muda wa miezi sita kabla ya mavuno kuvunwa baada ya upanzi.
Bwana Munya anaonya iwapo vijana hawatakumbatia kilimo, delta hii itakufa Mia michache inayokuja kwani mwaka wa wastani wa wakjlkma wa sasa ni mwaka hamsini na tisa.
“Katika mwaka wa elfu moja kenda mia na sabini, taifa la Kenya halikuwa na Ghana wa chakula lakini kuanzia mwisho mwisho was mwaka huo huo, tumekua tukishuhudia upungufu wa vyakula na kutufanya kununua chakula kutoka mataifa ya ughaibuni,”Anasema.
Anashangaa kwanini taifa linaagiza vyakula kutoka inje ilhali tunao mashamba ya kutonsha na idadi ya watu.
“Kile kinachotuumiza kwa sana no Kuwa hatutumii tecknolojia na ujuzi,” anasema Bwana Munya.
Bi Mwangi anaongeza kuwa watajadialiana na wakaaji waeneo hilo ndiposa wapate ekari mbili ndiposa kumaliza mradi wrote.
“Tunaomba serikali itupe shamba za serikali ambazo hazitumiki ili tupumguze garama ya kukomboa kutoka kwa watu wa kibknafsi,” Anasema Bi Mwangi.
Pia, mradi huo unatarajiwa kufaidi zaidi ya vijana 171,000 waliofuzu katika chuo watakaotoa mawaidha ya kisheria na kibayolojia.
“Serikali inafaa kuamrisha kila taasisi na shirika la serikali kununua bidha za shambani kutoka kwa vijana hawa ili wasiwe na tatizo la wateja,” anasema.
Mtaalamu wa Uchumi Ken Gichinga anasema kutokana na kampuni nyingi kufunga biashara humu nchini, watakaohitimu elimu ya chuoni mwaka huu wataumia zaidi katika harakati zao za kusaka nafasi za kazi.
“Hata kabla ya ugonjwa huu, uchumi wa Kenya haukuwa ukifanya vizuri. Vikundi hivi vinapaswa kuwekeza kwa sekta ambazo zitawapa kazi haraka,” akasema Bw Gichinga.
Anasema Benki Kuu ni sharti iongeze pesa kwenye mazingira ili nafasi za kazi zibuniwe kama hapo awali.