• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
MAONI: Bunge lina uwezo wa kuokoa Kenya kwa kuchangia kukabiliana na ufisadi

MAONI: Bunge lina uwezo wa kuokoa Kenya kwa kuchangia kukabiliana na ufisadi

NA KINYUA KING’ORI

Ufisadi umegeuka maradhi hatari yaliyokosa tiba Nchini,huenda wakenya wote tumeambukizwa ndwele hili.

Ukweli ni Kwamba taifa hili linapoteza pesa nyingi na kusababisha miradi mingi kukwama kutokana na visa vya ufisadi kuendelea kuongezeka na vinavyothibitishwa hupuuzwa tu.

Tumepoteza wakenya zaidi ya 300 majuzi kutokana na janga la mafuriko yanayoendelea kusababisha uharibifu na maafa makubwa katika historia ya Kenya,na viongozi kuanzia magavana hadi Rais Ruto hawaoneshi ishara ya kushtuka kiasi cha kushirikiana kutafuta suluhu la kudumu kuokoa raia wanaoteseka na watoto wao manyumbani baada ya shule kukosa kufunguliwa baada ya shule nyingi vijijini na mijini kuharibiwa vibaya na mafuriko.

Serikali inapaswa kuwa imeanza mikakati ya haraka kujenga upya madarasa yaliyoharibiwa na mafuriko,lakini ihakikishe fedha ambazo zimetengwa katika shughuli hizo zinatumika kwa uwazi bila ufujaji.

Taifa laweza kupona gonjwa la ufisadi ikiwa wabunge wetu watakubali kutekeleza majukumu yao kikatiba kwa manufaa ya umma bila kuzingatia maoni ya vinara wa vyama vyao vya kisiasa.

Bunge ni taasisi huru na muhimu kwa ustawi wa taifa hili na hivyo wanapaswa kukomboa uchumi na maendeleo kwa manufaa ya raia waliowachagua kuwa wakilishi wao Bungeni.

Wabunge wanastahiki kuhakikisha wanachunguza miradi ya umma na mawaziri serikalini wanatekeleza majukumu yao kwa uwazi bila ufujaji wa fedha za umma.

Jiulize! Je kwa nini barabara zilizotengewa fedha nyingi kuwekwa lami au kukarabatiwa zimebomoka au kuharibika kabisa kiasi cha kutopitika baada ya mvua kunyesha?.

Je,kwa nini madarasa yanayojengwa katika maeneo yote nchini kupitia fedha za NG-CDF yamebomoka,kuharibika au kusombwa na maji?.

Je, serikali ya kitaifa na Kaunti zimejiandaa vipi kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mafuriko?.

Ikiwa Bunge litaweza kutumia kasoro ambazo zimejulikana kupitia mvua wawe wazalendo kuwapa funzo maafisa wafisadi serikalini kuhakikisha wanawajibikia utepetevu.

Juzi,waliungana bila Siasa na kufaulisha hoja ya kumtimua Waziri wa kilimo Mithika linturi ambaye sasa atachunguzwa na kamati maalum kuhusiana na sakata ya mbolea ghushi.

Wabunge wana wajibu muhimu kuhakikisha raia wanapata dhamana ya pesa zao kupitia miradi bora na ubora wa fedha zao.

Wabunge,maseneta na madiwani washirikiane Sasa kuwatimua viongozi wafisadi kuanzia mawaziri,magavana na maafisa wa kaunti wanaojihusisha na Visa vya ufisadi kwa kusababishia taifa kupata hasara kwa kutekeleza miradi yenye viwango duni inayoathiri uchumi na ustawi.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti yaondoa marufuku ya kutumia fuo baada ya Hidaya...

Afueni kwa Wakenya madaktari hatimaye wakiridhia kusitisha...

T L