• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:55 AM
ALPHARAMA FC kujipima nguvu dhidi ya wakali wa KPL

ALPHARAMA FC kujipima nguvu dhidi ya wakali wa KPL

Na JOHN KIMWERE

ALPHARAMA FC imeapa kuwa haina la ziada mbali inalenga kujipima uwezo wake dhidi ya klabu kubwa ambazo hushiriki Ligi Kuu ya KPL bila kuweka katika kaburi la sahau Supa Ligi ya Taifa (NSL).

Kikosi hicho kinazidi kuzuru maeneo tofauti nchini kushiriki mechi za kirafiki kwenye jitihada za kujiweka bomba kukabili upinzani wowote katika Ligi ya Taifa Daraja la Pili msimu ujao.

Kocha wake, Stephen Orego anasema ”Kusema ukweli nashukuru wachezaji wangu wanaendelea kuonyesha wanaweza kwenye mapambano ya kirafiki licha ya kutoshiriki ligi yoyote msimu uliopita.” Anasema kuwa analenga kupimana nguvu na vikosi vya hadhi ya juu ili wachezaji wazidi kujifunza soka.

Kwenye ziara yake jijini Nairobi, Alpharama FC iliitandika Black Mamba kwa mabao 3-2 siku moja baada ya kunyoroshwa kwa mabao 3-2 na WYSA FC.

”Tuliamua kuzamia mechi za kirafiki ili wachezaji waendelee kukaa vizuri kwa ajili ya kurejea michezo ya ligi msimu ujao,” alisema na kuongeza kuwa vijana hao wanaendelea kufanya vizuri.

Kwenye mechi za hivi karibuni: Alpharama FC 3-2 Athi River United, Alpharama FC 4-2 KMTC, Alpharama FC 4-1 Katoloni FC, Alpharama FC 2-0 Makongeni United, Alpharama FC 1-1 Thika Allstars na Alpharama FC 1-0 Limuru Olympic.

Inajivunia wachezaji kama: Levy Simiyu, Hassan Gady (nahodha), Alex Sangala, Ambrose Imbusi, Clifford Barare, Emmanuel Mabonga na Boaz Odhiambo.

You can share this post!

Kinyago United yatolewa jasho kisha kulimwa

Wanaume wengi hunitaka kimapenzi ili wanipe ajira ya...

adminleo