• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 6:50 AM
Arsenal, Man City katika presha ya kujaza pengo lililofunguliwa na Liverpool

Arsenal, Man City katika presha ya kujaza pengo lililofunguliwa na Liverpool

LONDON, UINGEREZA

MANCHESTER City na Arsenal watakuwa mawindoni kupunguza presha ya kuachwa na Liverpool kwenye Ligi Kuu (EPL) watakapopepetana na Bournemouth na Newcastle leo usiku, mtawalia.

Nambari mbili Man-City wana alama 56, nne nyuma ya viongozi Liverpool. Wana mtihani unaokaa rahisi dhidi ya wenyeji Bournemouth.

Vijana wa kocha Pep Guardiola, wanaofukuzia taji la nne mfululizo la EPL na sita tangu 2017-2018, wana ushindi mara 18 na sare mbili katika michuano 20 dhidi ya Bournemouth.

Man-City pia hawajapoteza mechi 10 mfululizo msimu huu.

Inamaanisha Bournemouth (nambari 13) wana kibarua kigumu kuepuka kipigo, hasa kwa sababu pia wenyewe wanasuasua. Wamepiga sare tatu na kupoteza mara tatu katika michuano sita iliyopita.

Isitoshe, Bournemouth hawana ushindi katika mechi 12 dhidi ya timu iliyo katika mduara wa nne-bora.

Arsenal (tatu) wataalika Newcastle (nane) ugani Emirates wakitumai kujinyanyua baada ya kunyamazishwa 1-0 na Porto kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), Jumatano.

Takwimu za ana kwa ana za hivi karibuni zinaonyesha ni mechi inayoweza kuenda kivyovyote.

Hata hivyo, Arsenal watalenga kulipiza kisasi kichapo cha 1-0 katika mkondo wa kwanza ugani St James’ Park mwezi Novemba.

Vijana wa kocha Mikel Arteta walitoka 0-0 timu hizo zilipovaana Emirates mara ya mwisho Januari 2023.

Kabla ya hapo, Arsenal walikuwa wamezoa ushindi mara 10 na sare moja dhidi ya Newcastle.

Arteta hatakuwa na huduma za Gabriel Jesus, Takehiro Tomiyasu, Oleksandr Zinchenko na Jurrien Timber walio mkekani. Kiungo mkabaji Thomas Partey amerejea mazoezini.

Martin Odegaard amechangia katika kuzalishwa kwa magoli manne katika mechi mbili mfululizo ligini. Huenda anabeba ufunguo wa Arsenal kutwaa ushindi akisaidiana na Bukayo Saka na Gabriel Martinelli.

Anthony Gordon alizamisha Arsenal katika mkondo wa kwanza. Anaweza kusababisha madhara tena asipokabwa vizuri.

Newcastle pia wana silaha hatari beki Kieran Trippier na kiungo Bruno Guimaraes, ingawa bado watakosa majeruhi Callum Wilson, Alexander Isak, Nick Pope, Elliot Anderson, Matt Targett na Joelinton.

Ratiba ya LaLiga

(Leo – Granada vs Valencia (4.00pm), Barcelona vs Getafe (6.15pm), Alaves vs Mallorca (8.30pm), Almeria vs Atletico Madrid (11.00pm); Kesho – Cadiz vs Celta Vigo (4.00pm), Real Betis vs Bilbao (6.15pm), Las Palmas vs Osasuna (8.30pm), Real Madrid vs Sevilla (11.00pm); Jumatatu – Girona vs Rayo Vallecano (11.00pm).

Bundesliga

Union Berlin vs Heidenheim (5.30pm), Werder Bremen vs Darmstadt (5.30pm), Stuttgart vs Cologne (5.30pm), Monchengladbach vs Bochum (5.30pm), Bayern Munich vs Leipzig (8.30pm); Kesho – Eintracht Frankfurt vs Wolfsburg (5.30pm), Dortmund vs Hoffenheim (7.30pm), Augsburg vs Freiburg (9.30pm).

Serie A

Sassoulo vs Empoli (5.00pm), Salernitana vs Monza (8.00pm), Genoa vs Udinese (10.45pm); Kesho – Juventus vs Frosinone (2.30pm), Cagliari vs Napoli (5.00pm), Lecce vs Inter Milan (8.00pm), AC Milan vs Atalanta (10.45pm); Jumatatu – Roma vs Torino (8.30pm), Fiorentina vs Lazio (10.45pm).

Ligue 1

Lorient vs Nantes (7.00pm), Strasbourg vs Brest (11.00pm); Kesho – Lens vs Monaco (3.00pm), Le Harve vs Reims (5.00pm), Nice vs Clermont Foot (5.00pm), Toulouse vs Lille (5.00pm), PSG vs Rennes (7.05pm), Marseille vs Montpellier (10.45pm).

  • Tags

You can share this post!

Kidege Shakira hapumui ‘mafisi’ wakiwania tunda lake...

Vyama vya UDA na ODM vyang’ang’ania wanachama

T L