• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Arsenal wasambaratisha kasri la Crystal kwa ‘risasi’ tano

Arsenal wasambaratisha kasri la Crystal kwa ‘risasi’ tano

Na MASHIRIKA

ARSENAL wamefufua matumaini yao ya kusalia miongoni mwa wagombezi halisi wa taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2023-24 baada ya kuponda Crystal Palace 5-0 uwanjani Emirates.

Vijana hao wa kocha Mikel Arteta walishuka dimbani Jumamosi wakiwa na presha kali ya kujinyanyua baada ya kupoteza mechi tatu kati ya tano katika EPL mwishoni mwa mwaka wa 2023.

Wakicheza dhidi ya Palace, walikamilisha kipindi cha kwanza wakijivunia uongozi wa 2-0 kupitia bao la Gabriel Magalhaes aliyefunga kwa kichwa na la kipa Dean Henderson aliyejifunga kutokana na mpira wa kona.

Fowadi wa zamani wa Brighton, Leandro Trossard, aliwafungia Arsenal goli la tatu kabla ya Gabriel Martinelli kutokea benchi katika kipindi cha pili na kucheka na nyavu za Palace mara mbili.

Arsenal sasa wanakamata nafasi ya tatu jedwalini kwa alama 43 sawa na Aston Villa wanaofunga mduara wa nne-bora. Hata hivyo, wametandaza mchuano mmoja zaidi kuliko viongozi Liverpool (alama 45) na mabingwa watetezi Manchester City ambao pia wana pointi 43. Palace ni wa 14 jedwalini kwa alama 21 kutokana na mechi 21.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Shabana yapigwa na Ulinzi ugani Raila Odinga

Wachimbaji madini wapewa mafunzo kuepuka vifo migodini

T L