• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Arsenal yaingia sokoni kusaka beki wa kushoto ‘blanda’ za Zinchenko zikiwafika kooni

Arsenal yaingia sokoni kusaka beki wa kushoto ‘blanda’ za Zinchenko zikiwafika kooni

NA CECIL ODONGO

KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta, amesema kuwa lengo lake kuu katika kipindi cha usajili wa wachezaji Januari hii ni kumpata beki wa kushoto.

Arteta anataka beki wa kushoto kwa sababu wachezaji ambao wamekuwa wakihimili nafasi hiyo, wamekuwa wakikumbwa na majeraha huku wengine wakionyesha mchezo usioridhisha.

Beki Oleksandr Zinchenko amekuwa akikashifiwa kwa kufanya makosa kadhaa na alikosa kichapo cha 2-1 dhidi ya Fulham wikendi iliyopita kutokana na jeraha. Jakub Kiwior amekuwa akiokoa jahazi kwenye nafasi hiyo iila ameng’ang’ana sana ikizingatiwa yeye ni beki wa kati na hajazoea nafasi hiyo.

Kutokana na matatizo hayo, itabidi Arteta asajili beki wa kushoto hata kama ni kwa mkopo ili kuokoa jahazi hasa wakati huu ambapo timu hiyo imekuwa ikisuasua katika Ligi Kuu Uingereza (EPL) baada ya kuwa na mwanzo mwema.

Timu zimekuwa zikitumia udhaifu katika nafasi hiyo kuadhibu The Gunners. Arsenal pia imekuwa ikilenga sana kumsajili beki wa Real Sociedad Mark Zubimendi ambayo pia anaandamwa na Bayern Munich.

Katika safu ya mbele , Arsenal inamtaka Ivan Toney wa Brentford na winga wa Wolves Pedro Neto. Hii ni kwa sababu washambuliaji wa Arsenal wamekuwa wakilemewa kuyafunga magoli licha ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ndani ya kijisanduku.

  • Tags

You can share this post!

Watu ni kupambana na ‘githeri rasta’ Januari

Bodaboda waliochukuliwa wapachikaji mimba wawalinda...

T L