Michezo                                                
                                            
                                        Arsenal yapewa Bayern Munich hatua ya robo-fainali Uefa
 
                                                    
                                                        Arsenal yakutanishwa na miamba Bayern Munich katika hatua ya robo-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya; Manchester City kukwaana na Real Madrid nayo Atletico Madrid kupambana na Borussia Dortmund huku Paris Saint-Germain ikipewa FC Barcelona. PICHA | REUTERS                                                     
                                                NA REUTERS
KLABU ya Arsenal imekutanishwa na miamba Bayern Munich katika droo ya mechi za hatua ya robo-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (Uefa).
Kulingana na droo iliyofanywa Ijumaa, klabu nyingine ya Uingereza, Manchester City–ambao ndio mabingwa watetezi– itakwaana na Real Madrid ya Uhispania.
Nayo Atletico Madrid inatarajiwa kupambana na Borussia Dortmund huku Paris Saint-Germain ikipewa FC Barcelona.