Michezo

Baryan atwaa taji la KCB Kilifi Rally

August 17th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na GEOFFREY ANENE

MFALME wa Mbio za Magari za Afrika, Manvir Baryan, ameibuka mshindi wa duru ya nne ya kitaifa ya Kenya ya KCB Kilifi Rally, Jumamosi.

Baryan, ambaye amekuwa aking’ara katika mashindano ya Bara Afrika katika kipindi cha miaka miwili, lakini bila ufanisi mkubwa nyumbani, alibeba taji la Kilifi Rally kwa saa 1:50:50.

Dereva huyu alishirikiana na Drew Sturrock katika gari la aina ya Skoda Fabia. Walishinda

Alifuatwa na unyounyo na bingwa wa Safari Rally Baldev Chager na mwelekezi wake katika gari la Mitsubishi EVO10 (1:57:57) na mwenyeji Izhar Mirza akishirikiana na Kavit Dave katika gari la Mitsubishi Evolution (1:58:27), mtawalia.

Madereva wanane kati ya 23 walioanza mashindano hawakumaliza kutokana na matatizo mbalimbali akiwemo mshindi wa KCB Nakuru Rally Onkar Rai alitoka jukwaani katika nafasi ya kwanza Ijumaa usiku mashindano haya yalipoanza.

Madereva Piero Cannobio (Mitsubishi EVO10), Geoff Mayes (Land Rover), Adil Mirza (Mitsubishi EVO8), Raaji Bharij (Porsche 911), Hussein Malik (Mitsubishi EVO10), Naushad Kara (Subaru Impreza), Minesh Rathod (Mitsubishi Evolution 10) na Akbar Khan pia hawakukamilisha mashindano.

Baada ya Kilifi Rally, kuna Nanyuki Rally (Agosti 31 na Septemba 1), Simba Union Club (Oktoba 19-20), Rallye Sports Club (Novemba 9-10) na Eldoret (Novemba 23-24).