• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 12:36 PM
Benzema nafasi ya 5 kwa wafungaji bora Real

Benzema nafasi ya 5 kwa wafungaji bora Real

Na CHRIS ADUNGO

KARIM Benzema sasa anashikilia nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote kambini mwa Real Madrid, Uhispania.

Mabao mawili yaliyofungwa na fowadi huyo raia wa Ufaransa mnamo Juni 18 yalisaidia Real kuwazamisha Valencia kwa kichapo cha 3-0 kwenye Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Ushindi huo uliwasaza Real katika nafasi ya pili jedwalini kwa alama 62, mbili pekee nyuma ya viongozi Barcelona.

Benzema, 32, kwa sasa anajivunia kufunga jumla ya mabao 243 katika mashindano yote ambayo amewasakatia Real.

Idadi yake ya mabao imepiku ile iliyokuwa ikijivuniwa na Ferenc Puskas aliyefungia Real jumla ya magoli 242 kati ya 1958 na 1966.

Mabao yaliyofungwa na Benzema dhidi ya Valencia yalikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na fowadi wa zamani wa Chelsea, Eden Hazard. Bao jingine la Real ambao kwa sasa wananolewa na kocha Zinedine Zidane lilifumwa wavuni na kiungo Marco Asensio.

Hadi kufikia sasa, Cristiano Ronaldo ambaye huu ni msimu wake wa pili kambini mwa Juventus, angali anaongoza orodha ya wafungaji bora wa Real kwa mabao 450. Raul Gonzalez ni wa pili kwa mabao 323 huku Alfredo Di Stefano akishikilia nafasi ya tatu kwa magoli 308. Carlos Alonso Santillana anafunga orodha ya nne-bora kwa mabao 290.

Hazard aliyejiunga na Chelsea mnamo Juni 2019 kwa kima cha Sh21 bilioni, alipoteza nafasi nyingi za wazi licha ya kusalia peke yake uso kwa macho na kipa Jasper Cillessen. Real kwa sasa wanajiandaa kuvaana na Real Sociedad mnamo Juni 21, 2020.

  • Tags

You can share this post!

Bunge la Wajir laidhinisha mswada licha ya vurugu

Majeraha zaidi Arsenal

adminleo