• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Brewster ajiunga na Sheffield Utd

Brewster ajiunga na Sheffield Utd

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Rhian Brewster, 20, ameingia katika sajili rasmi ya Sheffield United kwa kima cha Sh3.2 bilioni.

Sogora huyo raia wa Uingereza amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano.

Brewster alikuwa sehemu ya kikosi cha Uingereza U-17 kilichotwaa Kombe la Dunia mnamo 2017. Akivalia jezi za Swansea City kwa mkopo, fowadi huyo alipachika wavuni jumla ya mabao 11 katika mechi 22.

Sheffield United, ambao waliambulia nafasi ya tisa ligini msimu uliopita wa 2019-20, hawakufunga bao lolote katika mechi tatu za kwanza za muhula huu.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga na Sheffield United huduma za Brewster zilikuwa zikiwaniwa na Aston Villa, Brighton, Burnley, Crystal Palace, Fulham na Newcastle United.

Mabao manane yalifunguwa na Brewster kambini mwa Uingerea wakati wa fainali za Kombe la Dunia za Under-17 yalimvunia taji la Mfungaji Bora wa kipute hicho kwa pamoja na kiungo mvamizi wa Manchester City, Phil Foden na Jadon Sancho wa Borussia Dortmund.

Brewster amethibitisha kwamba sasa amepona jeraha alilolipata mnamo Januari 2018 na kumweka nje ya kampeni nzima za msimu huo.

Hadi alipoondoka ugani Anfield, fowadi huyo alikuwa amewajibishwa na Liverpool mara nne, mara tatu kwenye Carabao Cup na mara moja kwenye gozi la Community Shield dhidi ya Arsenal mwishoni mwa Agosti 2020.

Jeraha linalouguzwa na Lys Mousset huenda likampa Brewster fursa ya kuwajibishwa na Sheffield United kwa mara ya kwanza dhidi ya Arsenal katika mechi ya EPL mnamo Oktoba 4, 2020 ugani Emirates.

Baada ya kuvaana na Arsenal, Sheffield United wameratibiwa kuchuana na Liverpool mnamo Oktoba 24 kabla ya kuwaalika Manchester City ugani Bramall Lane wiki moja baadaye.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Klopp Mane kupatikana na corona

Neymar afunga mawili na kusaidia PSG kuponda Angers 6-1