• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:47 AM
CAF yaizaba Gor faini ya Sh500,000 kwa kuzua ghasia Kasarani

CAF yaizaba Gor faini ya Sh500,000 kwa kuzua ghasia Kasarani

Na CECIL ODONGO

MABINGWA mara 17 wa KPL Gor Mahia wamepigwa faini ya Sh500,000 na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kutokana na rabsha zilizogubika mechi yao na Rayon Sports ya Rwanda ugani MISC Kasarani Agosti 2018.

K’Ogalo walipokezwa barua kutoka kwa CAF Jumanne Septemba 18 ikiwataka kulipa fedha hizo, mwezi mmoja tu baada ya kubanduliwa nje ya kipute hicho kufuatia ushinde wa 2-1 ugenini dhidi ya USM Algier na kichapo cha 2-1 mikononi mwa Rayon Sports nchini.

“Bodi ya nidhamu ya CAF imeamua kutoza faini klabu yenu Sh500,000 kutokana na vurugu za mashabiki wake,” ikasema sehemu ya barua hiyo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Gor Mahia Omondi Aduda alithibitisha kupokea barua hiyo kutoka kwa CAF na akawataka mashabiki kutorudia makosa kama hayo siku zijazo ili kuepusha klabu dhidi ya kukumbana na faini kama hizo.

“Tazama sasa tunalazimishwa kulipa faini ambayo hatukupangia kutokana na mashabiki wetu kuzua rabsha katika mechi dhidi ya Rayon Sports. Nawaomba mashabiki wetu wabadilishe mienendo yao ili kutuepusha dhidi ya kulipa gharama kubwa kama hizi,” akasema Bw Aduda.

You can share this post!

UEFA: Liverpool, Barcelona, Inter, Gala, Dortmund na...

Wakenya wamponda ‘Baba’ kwa kuunga mkono ushuru...

adminleo