Chumba kutetea ubingwa Tokyo Marathon
Na GEOFFREY ANENE
MKENYA Dickson Chumba atatetea taji lake la mbio za Tokyo Marathon hapo Machi 3, 2019 nchini Japan, waandalizi wametangaza.
Chumba aliibuka bingwa mwaka 2014 na 2018 na kumaliza makala ya mwaka 2015, 2016 na 2017 katika nafasi ya tatu.
Atakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa bingwa wa Berlin Marathon mwaka 2016 Kenenisa Bekele, ambaye huwa mwiba akiwa katika hali nzuri.
Mabingwa Marius Kipserem (Abu Dhabi Marathon), Nobert Kigen (Amsterdam Marathon), Gideon Kipketer (Mumbai Marathon) na Bedan Karoki (Ras Al Khaimah Half Marathon) ni Wakenya wengine watakaopigania taji la wanaume.
Malkia wa zamani wa Chicago Marathon Florence Kiplagat pamoja na mshindi wa Prague Half Marathon Joan Chelimo Melly na bingwa wa Gold Coast Marathon Ruth Chebitok ni Wakenya watajika pekee waliotoa ithibati ya kuwania taji la wanawake la Tokyo Marathon mwaka huu.
Orodha ya washiriki watajika wa Tokyo Marathon 2019
Wanaume na muda yao bora:
Kenenisa Bekele (Ethiopia) saa 2:03:03
Birhanu Legese (Ethiopia) 2:04:15
Dickson Chumba (Kenya) 2:04:32
El Hassan El Abbassi (Bahrain) 2:04:43
Seifu Tura (Ethiopia) 2:04:44
Nobert Kigen (Kenya) 2:05:13
Suguru Osako (Japan) 2:05:50
Gideon Kipketer (Kenya) 2:05:51
Marius Kipserem (Kenya) 2:06:11
Deme Tadu Abate (Ethiopia) 2:06:47
Bedan Karoki (Kenya) 2:07:41
Ryo Kiname (Japan) 2:08:08
Shogo Nakamura (Japan) 2:08:16
Yuki Sato (Japan) 2:08:58
Kenta Murayama (Japan) 2:09:50
Jo Fukuda (Japan) 2:09:52
Shohei Otsuka (Japan) 2:10:12
Daichi Kamino (Japan) 2:10:18
Wanawake na muda yao bora:
Ruti Aga (Ethiopia) saa 2:18:34
Feyse Boru Tadese (Ethiopia) 2:19:30
Yebrgual Melese (Ethiopia) 2:19:36
Florence Kiplagat (Kenya) 2:19:44
Shure Demise (Ethiopia) 2:20:59
Bedatu Hirpa (Ethiopia) 2:21:32
Mimi Belete (Bahrain) 2:22:29
Helen Tola (Ethiopia) 2:22:48
Rose Chelimo (Bahrain) 2:22:51
Ruth Chebitok (Kenya) 2:23:29
Honami Maeda (Japan) 2:23:48
Yuka Takashima (Japan) 2:26:13
Keiko Nogami (Japan) 2:26:33
Ababel Yeshaneh (Ethiopia) 2:33:10
Joan Chelimo Melly (Kenya) atashiriki kwa mara ya kwanza kabisa
Mao Ichiyama (Japan) atashiriki kwa mara ya kwanza kabisa