• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
DIMBA MASHINANI: Klabu mpya inayosaka udhamini kuwika gozini

DIMBA MASHINANI: Klabu mpya inayosaka udhamini kuwika gozini

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

NI mwaka mmoja tangu klabu ya Eleven Stars FC kuundwa kwa minajili ya kuinua vipaji vya soka vya wavulana na kina dada wa sehemu ya Maweni Gorofani, Kaunti ya Kilifi.

Mashabiki wa soka wa eneo hilo ambalo liko wadi ya Matopeni wanataka wahisani wajitokeze kuisaidia timu hiyo ili chipukizi wao wapate kushiriki kwenye Ligi ya Kaunti ya Kilifi msimu unaotarajia kuanza wakati wowote.

Mwanzilishi wa klabu hiyo, Kassim Ndecco ameambia Dimba kuwa wana mipango kabambe kuhakikisha wanashiriki kwenye ligi ya kaunti hiyo ili waweze kupigania nafasi ya kushinda na kupanda ngazi hadi Ligi ya Pwani Kaskazini.

“Ninawaambia mashabiki wetu kuwa tuko kwenye mikakati ya kuhakikisha tunashiriki ligi inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF),” akasema Ndecco.

Ndecco anasema Kocha Mkuu Wycliff Shivachi akisaidiwa na makocha wengine wawili, wameanza kuwaandaa wachezaji wao kwa kutumia masharti ya kujilinda na ugonjwa wa Covid-19.

“Wanasoka wetu wanafanya mazoezi ya binafsi, tukisubiri kufunguliwa kwa michezo na Waziri wa Michezo Amina Mohamed. Tunataka tukiingia ligi, tutambe na kupanda ngazi; hatutaki tubakie ligi hiyo msimu utakaofuatia,” akasema Ndecco.

Kocha Shivachi alisema ana matumaini timu yake kufanya vizuri katika ligi hiyo ya kaunti sababu amewashuhudia wanasoka wake kuwa wazuri na wenye ari ya kupanda ngazi mwaka hadi mwaka hadi kufikia Ligi Kuu ya Kenya.

“Vijana wangu wana hamu ya kucheza soka ya hali ya juu. Wanataka kuinua vipaji vyao waweze kucheza soka ya kulipwa huko ng’ambo mbali ni kuisaidia timu yao kutambulika kwa kufika kileleni mwa ligi kuu ya hapa nchini,” akasema kocha huyo.

Shivachi anasema ana kikosi imara chenye wanasoka wanaofuata mafunzo na ambao wana hamu ya kuyatekeleza yale wanayofunzwa wakiwa uwanjani. Nahodha wa timu hiyo ni Morris Ronald na naibu wake John Wellington.

Baadhi ya wachezaji ni Alli Nyika, Juma Kassim, Raphael Mwangome, Rodgers David, Mike Mwangura, Ruphus Rimba, Said Bust, Rashid Kawawa, Lewis Mazia, Rassy Ali na Harrison Ronald.

Mfadhili Mkuu, Martin Wangura amesema ana hamu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi itakayoshiriki na kuahidi akirudi Ulaya atafanya mipango ya kuitafutia misaada ili ijikimu kwa mavazi pamoja na gharama nyingine.

Wengine ni Issa Harrison, Quinton Kambu, Erick Chiwai, Emmanuel Edward, Rock Samuel, Elias Kilimo, Ebrahim Abubakar, Adam Jarred, Shebe Basti, Boy mangi, Herdson Ronald, Emmanuel Edward na Elvis Mwavita.

Mfadhili Mkuu wa timu hiyo, Martin Wangura anayeishi Uingereza amesema ana hamu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi itakayoshiriki na kuahidi akirudi Ulaya atafanya mipango ya kuitafutia misaada ili ijikimu kwa mavazi pamoja na gharama nyingine.

“Ninataka kuhakikisha Eleven Stars inafika mbali kisoka na ninataka kwa msimu wao wa kwanza, wapate ushindi. Nitakaporudi England, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha ninapata misaada ili timu hiyo itemize ndoto yaske ya kushinda ligi hiyo,” akasema Wangura.

Kassim Ndecco ambaye pia ni huifadhili timu hiyo alimshukuru Wangura kwa msaada wake wa mipira, jezi na pesa taslimu ambazo zinaisaidia timu kufanya safari nje ya eneo hilo la Maweni Gorofani.

“Msaada wake unatufanya tufike mbali kisoka,” akasema.

Tangu timu hiyo ianzishwe mwaka uliopita, imefanikiwa kushinda kikombe kilichotolewa na mfadhili wao Wangura na kwa wakati huu, inajitayarisha kushiriki kwenye dimba la Mwaganda Cup, linalodhaminiwa na Mwakilishi wa wasi hiyo, Victor Mwaganda.

You can share this post!

MBWEMBWE: Mkwasi huyu wa kutumbua majipu ya wapinzani...

Familia mbili Pwani zaitaka serikali izisaidie kupata jamaa...