• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:55 AM
Droo ya Raga za Dunia Hong Kong 2018-2019

Droo ya Raga za Dunia Hong Kong 2018-2019

Na GEOFFREY ANENE

ORODHA ya mataifa yatakayopigania tiketi ya kushiriki Raga za Dunia msimu 2018-2019 katika mashindano ya mchujo mjini Hong Kong, imetangazwa.

Mataifa 12 yatashiriki mchujo huo mapema Aprili. Bara Afrika litawakilishwa na Uganda na Zimbabwe, Guyana na Jamaica zinatoka Americas, Uruguay na Chile (Amerika Kusini), Papua New Guinea na Visiwa vya Cook (Oceania), Hong Kong na Japan (Asia) na Ujerumani na Jamhuri ya Ireland (Ulaya).

Droo itafanywa Machi 12 baada ya duru ya sita ya Raga za Dunia mjini Vancouver kuandaliwa nchini Canada. Mabingwa wa mchujo huo watajaza nafasi ya timu itakayomaliza Raga za Dunia za msimu 2017-2018 katika nafasi ya 15 (mwisho), ambayo itatemwa.

Zikiwa zimesalia duru sita Raga za Dunia za msimu 2017-2018 umalizike, Urusi ndiyo inashikilia nafasi hiyo ya 15 kwa alama nane kutoka duru nne za kwanza.

Uhispania, ambayo ilishinda mchujo wa mwaka 2017, iko katika nafasi ya 14 kwa alama 16.

Kenya inashiriki duru zote 10 za Raga za Dunia pamoja na Argentina, Australia, Canada, Uingereza, Fiji, Ufaransa, New Zealand, Urusi, Samoa, Scotland, Afrika Kusini, Uhispania, Marekani na Wales.

You can share this post!

Pipeline na Prisons wazuiwa kufanyia mazoezi Kasarani

Gor, Nzoia, Chemelil na Sofapaka zawika KPL

adminleo