Michezo

Furaha riboribo mfugaji akipigwa jeki kwa Sh10 milioni za Sportpesa

Na CECIL ODONGO July 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MKULIMA Dennis Kipkoech, 60  alikuwa ameasi kilimo kutokana na changamoto za kifedha lakini sasa ameelekeza macho yake katika kurejelea ufugaji wa ngómbe wa maziwa baada ya kuangukia kitita cha Sportpesa.

Hii ni baada ya kushinda Sh10 milioni kwenye Sportpesa Midweek Jackpot kutokana na ubashiri sawa wa mechi 13 kati ya idadi yote 17.

Kabla ya kuingilia kilimo na kuishia kulemewa kwa sababu ya kukosa pesa, Kipchoech alikuwa akichuna majanichai.

“Kwa hizi Sh10 milioni naenda Githunguri kuyabadilisha maisha yangu. Nitanunua ngómbe wa maziwa pamoja na shamba ili kupanda malisho pamoja na mimea yangu,” akasema Kipchoech akiwa amezidiwa na furaha akikabidhiwa hundi ya Sportpesa.

Kuwahi hela hizo haikuwa rahisi kwa kuwa aliweka ubashiri mara mbili, mmoja ikikosa kutimia na ubashiri wa pili ambao hakumakinikia ndio ukampa Sh10 milioni.

Hata hii aliyoishinda ilijaa mchecheto kwa kuwa kuna mechi ambayo mmoja wa wachezaji alikuwa amepewa kadi nyekundu na nusura matokeo yabadilike kisha kuathiri ubashiri wake. Kipkoech sasa amekuwa wa saba kushinda Sportpesa Midweek Jackpot mwaka huu.

“Ningepata pesa hizi wapi kama hata siku hizi kupata mtu wa kukopesha Sh10,000 ni ngumu? Nashukuru sana nilifanikiwa,” akaongeza.

Kando na Sportpesa Midweek Jackpot, kuna Jackpot Kuu ya Sportpesa (Sportpesa Mega Jackpot) ambayo inaanza Jumamosi hii kwa kima cha Sh421, 326,863.

Wale ambao nao watafanikiwa kubashiri mechi 12,13, 14, 15 au 16 kati ya 17 wataangukia bonasi.