• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Fursa kwa Rotich na Masai kutawala Hamburg Marathon

Fursa kwa Rotich na Masai kutawala Hamburg Marathon

Na CHRIS ADUNGO

WANARIADHA Lucas Rotich na Magdalyne Masai (saa 2:26:02) sasa wana fursa ya kuboresha matokeo yao ya mwaka 2019 katika mbio za Hamburg Marathon ambazo waandalizi wamethibitisha kwamba zitaandaliwa Septemba 13, 2020.

Rotich aliambulia nafasi ya tano kwa muda wa saa 2:09:48 mwaka jana katika mbio hizo zilizotawaliwa na Waethiopia Tadu Abate (2:08:25) na Ayele Abshero (2:08:26) waliochukuwa nafasi mbili za kwanza katika kitengo cha wanaume.

Katika kategoria ya wanawake, Masai (2:26:02) aliambulia nafasi ya pili nyuma ya Dibabe Kuma wa Ethiopia huku Mkenya mwingine, Veronica Nyaruai akimaliza wa nne kwa muda wa saa 2:29:14.

Jumla ya wanariadha 10,000 wanatarajiwa kushiriki mbio za mita 42 za kivumbi hicho huku wengine 4,000 wakinogesha mbio za kilomita 21 za mashindano hayo ya Hamburg, Ujerumani. Washiriki wote watafanyiwa vipimo vya corona kabla ya kushuka ugani.

“Mikakati mingi ya kiafya imewekwa katika juhudi za kufanikisha kivumbi hicho cha Septemba 13. Tunapania kukamilisha shughuli za maandalizi kwa upande wa miungo-msingi kufikia mwisho wa Agosti,” akasema mkurugenzi wa mbio hizo Frank Thaleiser.

Mbio za Hamburg Marathon zilikuwa awali zimeratibiwa kuandaliwa Aprili 19, 2020 kabla ya kuahirishwa kutokana na janga la corona. Jumla ya wanariadha 30 pekee wa haiba kubwa zaidi katika mbio za mita 42 na 21 duniani watashiriki makala ya mwaka 2020.

You can share this post!

Guendouzi aonywa kwa ukosefu wa nidhamu

Ongeri achaguliwa mwenyekiti wa CPAIC

adminleo