• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
Gor Mahia walilia msaada wa fedha tena

Gor Mahia walilia msaada wa fedha tena

Na CECIL ODONGO

HALI si hali katika kambi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu (KPL) Gor Mahia ambao wanakumbwa na uchechefu wa fedha baada ya wachezaji kukosa kulipwa mshahara wa miezi miwili.

Mwenyekiti wa vigogo hao Ambrose Rachier mnamo Jumatatu alieleza Taifa Leo kwamba hali imekuwa ngumu kiasi kwamba baadhi ya wachezaji wanaelekea kufungiwa nyumba kwa kukosa kulipa kodi huku familia zao zikiteseka kwa kukosa mahitaji muhimu ya kimsingi.

“Kwa kweli hatuna namna kabisa na mbele ni giza totoro. Wanasoka wetu wako njaa na hatujui ni lini tutapata pesa za kuwalipa kwa sababu hatuna mdhamini. Wako njaa, familia zao zinaumia na motisha kambini ipo chini mno. Tunaomba msaada ili kuinuka kidogo,” akasema Rachier.

Mapito haya yanajiri huku K’Ogalo ikitarajiwa kuvaana na USM Algier kwenye mechi ya mkondo wa pili wa Klabu Bingwa Afrika(CAF) Jumapili hii baada ya kulemewa 4-1 ugenini mnamo Septemba 15.

Vigogo hao wa soka wa Algeria wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa mchana ili kudumisha ushindi wao huku K’Ogalo wakitarajiwa kufunga angalau mabao matatu na iombe wasifingwe ndipo wapate nafasi ya kusonga hadi hatua ya makundi.

Kuchangia

Akizungumzia madhila hayo, Afisa Mkuu Mtendaji wa K’Ogalo Lordvick Aduda naye aliwaomba mashabiki wa K’Ogalo waingie mifukoni ili kuchangia timu hiyo ndipo wapate angalau fedha kidogo za kuwanusuru wachezaji.

“Nawaomba mashabiki wachangie timu yetu kwa sababu mambo ni mabaya na sisi hatuwezi kumudu kuwalipa mishahara yao. Tunahitaji Sh10 milioni kulipa malimbikizi ya mshahara wao wa miezi miwili na pia Sh2 milioni kugharimia mechi ya nyumbani dhidi ya USM Algier. Hatuna pesa wala hakuna mahali tutazipata ndiposa tunategemea michango yao hata kama hatutafikisha kiasi kinachohitajika,” akasema Aduda.

Aidha alifunguka na kusema ni kupitia hisani tu ya baadhi ya mashabiki ambapo K’Ogalo ilisafiri hadi Machakos kuchapana na KCB kwa mechi ya KPL wikendi iliyopita na sasa mashabiki.

  • Tags

You can share this post!

Allegri au Xavi kutua Barca endapo kocha Ernesto atatimuliwa

Mapuuza yazua mauti shuleni

adminleo